"Nimemsikia Zaka Zakazi akisema ubingwa wetu wa kupewa, nawaheshimu sana Azam lakini wasisingizie tulibebwa, hii ni kukosa heshima watu tumeshinda back to back.

"Nimshukuru sana kocha wa Yanga Luc Eymael amekuwa mtu wa kwanza kumpigia simu kocha Sven kumpongeza kwa kutwaa ubingwa pia GSM amenipigia simu na kutupongeza pia".

"Sisi Azam ni wapinzani wetu ndani ya dakika 90' na si zaidi ya hapo. Tunawaheshimu Azam kama vile ambavyo tunawaheshimu Yanga ... lakini mtu kupata usemaji juzi basi anataka umaarufu. 

✍️Haji Manara -Afisa Habari SimbaSc .
==============================
Zaka Zakazi Ameamua Kumjibu hivi ...

HOJA KWA HOJA

1. Kuhusu kuwaponda mabingwa.

Yawezekana ulihadithiwa na mtu ambaye hakuelewa nilichokisema, au ulisikia ukiwa kwenye mhemko mkubwa sana.

Sikuwaponda mabingwa na wala sikuwagusa popote, zaidi ya kuwapongeza. Niliwapongeza mapema, mara tu baada ya mchezo... tena kupitia vyombo vya habari na kupitia akaunti binafsi ya Instagram. 

Lakini baada ya pongezi, nilitoa wito kwa waamuzi msimu ujao wafanye vizuri zaidi ya msimu huu ili bingwa asichafuliwe ubingwa wake kwa makosa yao.

Msimu huu ulikuwa moja ya misimu ambayo waamuzi wamefanya vibaya sana kiasi cha kamati ya waamuzi ya TFF kuvunjwa katikati ya msimu.

Kwa hiyo kusema waamuzi wajitahidi kupunguza makosa, ni kuwachafua mabingwa?

Au wewe hutaki waamuzi wakumbushwe kufanya vizuri?

2. Kuhusu kufungwa na Kagera.

Hivi watu husahau walilotoka? Kwani nani hajawahi kufungwa na Kagera? 

Aliyewapeleka Simba FIFA 2017, alikuwa nani?

Aliyesababisha makamu bingwa wa 2016/17 kususia tuzo za Vodacom ni nani?

Aliyesababisha kung'olewa viti uwanja wa taifa kwa mara ya kwanza kwenye historia ya uwanja huo mwaka 2013, alikuwa nani? 

Aliyetoboa tundu 2018 pale uwanja wa taifa ni nani?

1997 aliyewanyima Simba ubingwa pale Kaitaba alikuwa nani?

Leo hii Azam FC kufungwa na Kagera ndiyo kipimo?

3. Kuhusu wafungaji.

Kipimo cha ubingwa siyo lazima iwe mabao ya kinara wa orodha ya wafungaji bora.

Msimu wa 2011/12, Simba walikuwa mabingwa, na John Bocco wa Azam FC alikuwa na mabao 19.

Kinara wa mabao wa Simba alikuwa Emmanuel Okwi aliyefunga mabao 12.

Mabao mawili kati ya hayo, aliyafunga siku ya mwisho ya msimu, katika ushindi wa 5-0 dhidi ya Yanga.

Mabao 5 kati ya hayo yalikuwa ya penati... kwa hiyo Simba hakustahili kuwa bingwa?

Ni kweli, mfungaji bora wa Azam FC hadi sasa ana mabao 8, lakini hajafunga hata moja la penati...na ligi bado haijaisha.

ZAKAZAKAZI -Afisa Habari Azam Fc . #Nyakahiyo 
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: