Mwenyekiti wa kikao cha menejimenti Kamishna Mhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo (kushoto) akiongoza kikao maalum cha Menejimenti kilichofanyika leo jijini Dodoma ambapo pamoja na mambo mengine walipata fursa yakusikiliza wasilisho kutoka kwa kikoasi kazi kilichokwenda China kujifunza juu ya namna gani Tanzania inaweza kunufaika na zao la miti kutokana na uvunaji wa utomvu kutoka kwenye miti ya kupandwa (pines) pasipo kuhatarisha biashara ya mbao. Kikosi kazi hicho kiliongozwa na Prof. Rogers Malimbwi kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine Morogoro (SUA) ambaye alisema bado wanaendelea na tafiti ambayo itabainisha mambo mbalimbali ikiwepo kuonesha kama utomvu ukawa unalipa zaidi ya zao la miti . Kulia pichani ni Naibu Kamishna wa Huduma Saidizi, Emmanuel Wilfred.
Picha ya pili hadi tano ni wajumbe wa kikao hicho wakiendelea na kikao.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: