Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana, na wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama (MB)akitoa Tuzo kwa mwajiri bora wa mwaka 2019 David Magese wakati wa hafla yaTuzo ya mwaajiri bora wa mwaka 2019 iliyoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) katika Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam jana hafla hiyo iliyoudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo Naibu Waziri wa Stella Ikupa (MP) pamoja na Taasisi mbalimbali. Wanaoshuhudia kushoto ni Mkurugenzi wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Dkt. Aggrey Mlimuka na Mwenyekiti wa Bodi wa chama hicho Jayne Nyimbo.
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Jenista Mhagama amewataka waajiri muajiri kwa kuzingatia usawa wa kijinsia,na mpinge unyanyasaji wa kijinsia mahala pa kazi.Wanawake wana haki sawa na wanaume mahala pa kazi.
Hayo ameyasema wakati wa utoaji wa tuzo za waajiri bora kwa mwaka 2019 zilizofanyika usiku wa Kuamkia Desemba 19 mwaka huu na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu - Watu wenye ulemavu Stella Ikupa na makampuni wanachama na washiriki.
Tuzo hizo zilianza mwaka 2005 chini ya Chama cha Waajiri Tanzania ATE na zikiwa zinaboreshwa kila mwaka kwa kuongezeka kwa vinyang'anyiro vya kuwania tuzo tuzo hizo na kufikia 20.
Katika ushindi wa jumla Tanzania Breweries Limited (TBL) waliweza Kuibuka kinara na kushika nafasi ya kwanza, wakifuatiwa na Geita Gold Mines na wa tatu wakiwa Puma Energy.
Amesema, Mafanikio yapatikanayo mahali pa kazi yanategemea mkururo wa mambo mengi mno. Wakati tunapofikiri kuhusu haki za wafanyakazi, Basi wafanyakazi nao sharti watathimi wajibu wao mahala pa kazi. Hakuna haki bila wajibu.
Jenista amewakumbusha wafanyakazi kuhudhuria mafunzo mbalimbali endelevu ili kuongeza ujuzi na ufanisi katika kuendana na Kasi ya mabadiliko ya maendeleo na mwakani angependa kuona taasisi za sekta ya umma zinashiriki kwenye tuzo hizi za waajiri.
"Nimeshuhudia tukio la ugawaji tuzo hii ya waajiri bora kwa miaka mitatu sasa, ama kweli, Ushindani huwa ni mkubwa mno. Huwa siondoki bure kwenye tuzo hii, huwa najifunza kitu," Jenista
Aidha, amesema silimia 56 ya nguvu kazi nchini ni vijana. Wakati wa kuwashirikisha Vijana katika kazi na mambo mengine mtambuka ni sasa. Waajiri toeni fursa kwa vijana ili wajifunze, wajiajiri na kuajiri vijana wenzao. Vijana ni Taifa la leo
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu - Watu wenye ulemavu Stella Ikupa amewashukuru ATE kwa juhudi kubwa wanazofanya kwa kuwaunga mkono watu wenye ulemavu nchini. Changamoto bado zipo, wanajitahidi kuzitatua ili kusudi wasimuache mtu nyuma.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya ATE, Jayne Nyimbo amesema wanaamini ili kufikia mafanikio hasa katika nyanja za kiuchumi na kijamii, sharti kuzingatia mgawanyo sawa wa raslimali zetu nchini kwa watu wote. Kwa kuzingatia hilo, ATE wanaendelea kutekeleza Programu Maalumu (Female Future Programme) ambayo lengo lake ni kuhakikisha wanawajengea uwezo wanawake katika nyanja mbalimbali na hivyo kuwawezesha kushika ngazi za uongozi katika Taifa letu.
Amesema, Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2019 ambayo siyo tu itasaidia katika kuhamasisha waajiri katika kuonesha matendo mema bali pia kuongeza tija na ushindani mahali pa kazi.
Aidha, Afisa Mtendaji Mkuu wa ATE, Dkt Aggrey Mlimuka amesema tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka ni zoezi lililoanzishwa na kuendeshwa kila mwaka na Chama cha Waajiri Tanzania tangu mwaka 2005. Kwa miaka kadhaa tuzo hizi zimehamasisha makampuni wanachama kuweka juhudi katika masuala ya ajira na usimamizi wa rasilimali watu kama msingi mkakati wa makampuni yao kujenga nguvu kazi yenye ujuzi, furaha, ushindani, na yenye kushiriki kikamilifu katika uzalishaji.
Mlimuka ameeleza kuwa, kutokana na mapendekezo waliyopokea Kutoka kwa Waziri Jenista katika tuzo za mwaka jana, wadau na wataalamu wetu mbalimbali, tuzo ya mwajiri bora kwa mwaka huu 2019 imekuja na vipengele vipya vitatu (3) na kufanya kuwa na Jumla ya vipengele 38 kutoka vipengele 35 tulivyokuwa navyo mwaka jana.
" Vipengele vilivyoongezeka ni Mwajiri Bora anayeendaleza Mafunzo ya Ujuzi wa Kazi kwa wahitimu (Internship), Mwajiri Bora anayetoa mafunzo ya Uanagenzi (Apprentiship), Mwajiri Bora anayezingatia Haki Rasilimali ijulikanavyo kama Local Content."
Pia, amesema Lengo la kuongeza vipengele hivi ni kuendelea kuziboresha tuzo hizo na kuongeza ushindani miongoni mwa washiriki na pia kujaribu kugusa kila eneo ambalo litaleta tija katika ukuzaji na uendelezaji wa rasilimali watu katika maeneo ya kazi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana, na wenye Ulemavu Jenista Mhagama (MB)akihutubia wageni waalikwa wakati wa hafla yaTuzo ya mwaajiri bora wa mwaka 2019 iliyoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) katika Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam jana hafla hiyo iliyoudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana, na wenye Ulemavu Stella Ikupa (MP) pamoja na Taasisi mbalimbali.
Mwenyekiti wa Bodi ya Chama cha Waajiri Tanzania ATE, Jayne Nyimbo akitoa taarifa fupi wakati wa hafla yaTuzo ya mwaajiri bora wa mwaka 2019 iliyoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) katika Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam jana hafla hiyo iliyoudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo Naibu Waziri wa Stella Ikupa (MP) pamoja na Taasisi mbalimbali.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu - Watu wenye ulemavu Stella Ikupa akitoa neno la shukrani kwa Chama cha Waajriri ATE kwa juhudi kubwa wanazofanya kwa kuwaunga mkono watu wenye ulemavu nchini.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi TUCTA Said Wamba akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi na kuwashukuru Chama cha Waajiri Tanzania ATE kwa kutambua mchango wa wafanyakazi wawapo mahala pa kazi. Hayo ameyasema wakati wa utoaji tuzo kwa waajiri bora kwa mwaka 2019.
Mkurugenzi Mtendaji Puma Tanzania Dominic Dhanah akielezea masuala mbalimbali waliyoweza kuyafanya ndani ya mwaka 2019 ikiwemo kusaidia zoezi la upasuaji wa watoto wenye matatizo ya moy kwenye taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana, na wenye Ulemavu Mh. Stella Ikupa (katikati), akitoa tuzo kwa mwajiri bora wa mwaka 2019 kwa nafasi ya mshindi wa pili Geita Gold mines, Elizabeth Karua wakati wa hafla yaTuzo ya mwaajiri bora wa mwaka 2019 iliyoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) katika Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam jana hafla hiyo iliyoudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo Naibu Waziri wa Stella Ikupa (MP) pamoja na Taasisi mbalimbali. anaeshuhudia (kulia), ni Mwenyekiti wa Bodi wa Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE), Jayne Nyimbo.
Taasisi mbalimbali zikipokea tuzo wakati wa hafla yaTuzo ya mwaajiri bora wa mwaka 2019 iliyoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) katika Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam jana hafla hiyo iliyoudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo Naibu Waziri wa Stella Ikupa (MP) pamoja na Taasisi mbalimbali.
Toa Maoni Yako:
0 comments: