Katika kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka, Kamanda wa Kikosi cha Polisi Tazara (DPC) Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Advera Bulimba amewataka wananchi kutoa taarifa za wahalifu wanaowaibia abiria wanaosafiri na treni za reli ya tazara na wale wanaohujumu reli hiyo kwa kung’oa mataruma ya reli.
Kamanda Bulimba amesema kikosi chake kimejipanga vizuri kuhakikisha wanalinda miundombinu ya reli na kuhakikisha usalama wa abiria wanaosafiri kupitia reli hiyo wanakua salama wakati wote wa safari yao.
Ameongeza kuwa, wapo baadhi ya watu wasio waaminifu ambao hupenda kutumia kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka kujipatia kipato kisicho halali kwa kuwaibia abiria ama kuhujumu njia ya reli.
Aidha , kamanda bulimba amesema kuwa kikosi kimejipanga vizuri na tayari askari wa intelijensia, makachero na askari wa mbwa wamesambazwa maeneo mbalimbali ya kikosi hicho kuanzia tazara dar es salaam hadi tunduma.
Ametoa onyo kali wenye tabia za kihalifu kuacha mara moja na atakaethubutu kufanya uhalifu wowote watamchukulia hatua kali za kisheria.
Aliongeza kuwa Tazara ni moja ya chanzo cha kuingiza mapato ya nchi, na ili kufikia mafanikio hayo, ni lazima usalama wa mali na watu wanaotumia reli ya tazara uimarishwe na ndi maana kikosi hichi kipo na kipo imara na watahakikisha mapato yanayotokana na reli ya tazara hayata hujumiwa na mtu yeyote.
Katika kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka, Kamanda wa Kikosi cha Polisi Tazara (DPC) Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Advera Bulimba amewataka wananchi kutoa taarifa za wahalifu wanaowaibia abiria wanaosafiri na treni za reli ya tazara na wale wanaohujumu reli hiyo kwa kung’oa mataruma ya reli.
Kamanda Bulimba amesema kikosi chake kimejipanga vizuri kuhakikisha wanalinda miundombinu ya reli na kuhakikisha usalama wa abiria wanaosafiri kupitia reli hiyo wanakua salama wakati wote wa safari yao.
Ameongeza kuwa, wapo baadhi ya watu wasio waaminifu ambao hupenda kutumia kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka kujipatia kipato kisicho halali kwa kuwaibia abiria ama kuhujumu njia ya reli.
Aidha , Kamanda Bulimba amesema kuwa kikosi kimejipanga vizuri na tayari askari wa intelijensia, makachero na askari wa mbwa wamesambazwa maeneo mbalimbali ya kikosi hicho kuanzia Tazara Dar es Salaam hadi Tunduma.
Ametoa onyo kali wenye tabia za kihalifu kuacha mara moja na atakaethubutu kufanya uhalifu wowote watamchukulia hatua kali za kisheria.
Aliongeza kuwa Tazara ni moja ya chanzo cha kuingiza mapato ya nchi, na ili kufikia mafanikio hayo, ni lazima usalama wa mali na watu wanaotumia reli ya tazara uimarishwe na ndi maana kikosi hichi kipo na kipo imara na watahakikisha mapato yanayotokana na reli ya tazara hayata hujumiwa na mtu yeyote.
Toa Maoni Yako:
0 comments: