Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Jamii kutoka Mamlaka ya maji safi na maji Taka Dar es Salaam (DAWASA), Neli Msuya akitoa maelezo kuhusu kazi zinazofanywa na Mamlaka hiyo kwa wananchi waliotembelea banda hilo wakati wa maonesho ya wafanyabiashara yaliyofanyika katika viwanja vya Mlimani City jijini Dar es Salaam
Maofisa wa Mamlaka ya maji safi na maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) wakiendelea kutoa huduma kwenye banda la mamlaka hiyo wakati wa maonesho ya wafanyabiashara yaliyofanyika katika viwanja vya Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Ofisa wa Mamlaka ya maji safi na maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) Carolyn Njuju akitoa maelezo kwa baadhi ya kazi zinazotolewa kwa mshereheshaji Taji Liundi (wa pili kushoto) wakati wa maonesho ya wafanyabiashara yaliyofanyika katika viwanja vya Mlimani City jijini Dar es Salaam
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Jamii kutoka Mamlaka ya maji safi na maji Taka Dar es Salaam (DAWASA), Neli Msuy(kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na maofisa wa DAWASA wakati wa maonesho ya wafanyabiashara yaliyofanyika katika viwanja vya Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Huduma zikiendelea kutolewa kwenye banda la DAWASA.
Mamlaka ya maji safi na maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) wameshiriki maonesho ya kufanya malipo ya Serikali kwa kutumia mtandao wa Vodacom Tanzania yaliyoandaliwa na mtandao huo.
Maonesho hayo yameanza tarehe 26 hadi 30 Septemba yakifanyika katika viwanja vya Mlimani City leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Jamii kutoka Mamlaka ya maji safi na maji Taka Dar es Salaam (DAWASA), Neli Msuya amesema maonesho hayo yamekuja kuwawezesha watanzania kulipa malipo mbalimba kwa kutumia mtandao wa Vodacom.
DAWASA ni moja ya wateja wakubwa wa mtandao huo ambapo bili za maji utaweza kulipa kupitia mtandao wa Vodacom kwa njia rahisi na bila malipo yoyote.
Huduma zingine zinazotolewa na Mamlaka hiyo ni maunganisho mapya na kulipa bili za wateja. Mamlaka hiyo imehaidi kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja wao pamoja na kuweka mifumo rahisi na rafiki ambayo itawasaidia wateja kuifikia huduma kwa urahisi.
Toa Maoni Yako:
0 comments: