Mtumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Hilder Rugemalira akitoa hoja wakati wa kikao kati ya viongozi na Watumishi wa Wizara hiyo Jijini Dodoma.
Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakisikiliza hoja mbalimbali zilizokuwa zikitolewa katika kikao cha Watumishi wa Wizara hiyo Jijini Dodoma
Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Alfred Dede akitolea ufafanuzi baadhi ya hoja zilizoibuliwa wakati wa kikao cha Watumishi wa Wizara hiyo ambacho kiliongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Doto James (hayupo pichani), Jijini Dodoma.
Mhasibu Mkuu wa Serikali, Bw. Francis Mwakapalila akijibu hoja katika kikao kati ya viongozi na Watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango kilichofanyika Jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Adolf Ndunguru akifafanua jambo wakati wa kikao Kati ya Viongozi na Watumishi wa Wizara hiyo kilichofanyika Jijini Dodoma, ambapo Watumishi waliaswa kufanya kazi kwa bidii na weledi.
Na Josephine Majura, WFM, Dodoma.
Watumishi wa Wizara ya Fedha ya Mipango wametakiwa kuzingatia Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma katika kutekeleza majukumu yao.
Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Doto James wakati wa kikao cha watumishi wa Wizara hiyo.
Bw. James alisema kuwa watumishi wote wanawajibu wa kufanya kazi kwa ufanisi na weledi na kwa kuzingatia nidhamu, maadili, sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa Umma.
“Ni wajibu wa kila mtumishi kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi wote wanaohitaji huduma katika Wizara yetu” Alisema Bw. James.
Aidha Bw. James aliwapongeza Watumishi wa Wizara hiyo kwa kazi wanazozifanya hususan kazi ya uandaaji wa Bajeti Kuu ya Serikali iliyopishwa na Bunge hivi karibuni na kuwataka waendelee kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa Bajeti hiyo.
Kwa upande wa Watumishi wa Wizara hiyo waliupongeza uongozi wa Wizara hiyo kwa kutenga muda wa kuzungumza nao na kusikiliza changamoto mbalimbali zinazo wakabili pamoja na kuzitolea ufafanuzi.
Waliahidi kutatekeleza maelekezo yote aliyotolewa kwa uadilifu ili kuongeza ufanisi wa kazi kwa maendeleo ya nchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments: