Mbunge  wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu, akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana Kijiji cha Mtavira Kata ya Makilawa wilayani Ikungi mkoani Singida.
 Wasanii wakitoa burudani kwenye mkutano huo
 Mbunge  wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu, akicheza sanjari na wasanii.
 Mkutano ukiendelea
 Wananchi wakinyoosha mikono kuipongeza Serikali kwa kuwapelekea maendeleo
 Watoto wakiwa juu ya miti wakimsikiliza mbunge wao
Mkutano ukiendelea

Na DottoMwaibale, Singida.

MBUNGE wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu anatafuta sh.milioni 480 kwa ajili ya kuchimba visima virefu vya maji katika vitongoji 12 vilivyopo Kata ya Makilawa wilayani Ikungi mkoani Singida.

Akizungumza jana katika mkutano wa hadhara wenye lengo la kuzungumzia miradi ya maendeleo iliyofanyika katani hapo pamoja na kujua changamoto zilizopo Kingu alisema wananchi waliopo mji wa Mtavira wameanza kupata maji hadi kufikia hatua ya kuosha magodoro.

"Hapa Mtavira mnapata maji mengi kupitia mradi wa Tanjet sasa hivi naelekeza nguvu zangu kupeleka maji katika vitongoji 12 vya kata hii ambapo nitachimba visima 12 vyenye thamani ya sh.milioni 480 pamoja na ujenzi wa sekondari" alisema Kingu.

Kingu alivitaja vitongoji hivyo kuwa ni Magohana A,  Magohana B, Itulu, Kazizi, Munyu, Mpembu, Majengo, Mteva Kati, Songambele, Kasela, Kinyalambe na Darajani.

Akizungumzia kuhusu ujenzi wa sekondari alisema kwa kuanza atachangia mifuko ya saruji 150 huku madiwani wakiahidi kutoa mifuko 10 tu.

Kingu alisema miradi yote hiyo inafanyika kwa msaada mkubwa wa Rais Dkt. John Magufuli baada ya kuziba mianya ya fedha za serikali ambazo zilizokuwa zikitumika vibaya na mafisadi.

Aliongeza kuwa katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Serikali ya Rais Dkt.John Magufuli miradi mingi ya maendeleo imefanyika na mingine inaendelea kujengwa.

Alisema katika jimbo la Singida Magharibi baadhi ya miradi mikubwa iliyofanyika ni ya maji na ujenzi wa vituo vya afya vya kisasa Kata ya Sepuka na Ihanja ambacho kinavifaa tiba vya kisasa na wameajiriwa madaktari bingwa wanaotoa huduma za upasuaji kwa wananchi kutoka kata mbalimbali za jimbo hilo.

Kingu aliwahimiza wananchi kutunza miundombinu ya miradi hiyo baada ya kukamilika na kueleza kuwa itakuwa haina maana miradi iliyogharamiwa na serikali kwa fedha nyingi ikaachwa iharibike.

Diwani wa Kata ya Makilawa Hassan Mtakii alipongeza jitihada zinazofanywa na Serikali pamoja na mbunge huyo za kuwaletea maendeleo wananchi wa kata hiyo na nchi nzima kwa ujumla.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: