Mkurugenzi wa ZOOM Tanzania Mili Rughani (juu) akiongea na wanahabari katika mkutano.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko Stephen Swai (kwana kushoto) akizungumza wakati wa mkutano na wanahabari. 
Mkuu wa Kitengo cha Masoko Stephen Swai akifafanua jambo kwa wanahabari.

Tangu kuanzishwa kwake, Zoom Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika uvumbuzi wa jinsi ya kukutanisha watu na fursa mbalimbali. Kuanzia ujio wa kurasa za njano za digitali mwishoni mwa miaka ya 2000, mpaka kuanza kwa mtandao unaosaidia mauzo na manunuzi ya mtandaoni, Zoom Tanzania imejikita katika kuboresha jinsi inavyokutanisha wauzaji na wanunuzi kupitia mtandao wake.

Ili kubakia katika maono yake, Zoom Tanzania inaendelea kuboresha jinsi inavyofanya biashara, ili kila Mtanzania aweze kuuza kitu chochote. Hii itakuza biashara ya kifungu cha mnunuzi kwenda kwa mnunuzi (C2C) nchini kwa kutengeneza nafasi rafiki na salama kwa mtu wa kawaida asiyekuwa mfanyabiashara kuuza vitu asivyovihitaji mtandaoni.

Hii Inamaana Gani?

Wauzaji wote, wafanyabiashara na wasio wafanyabiashara, wanaweza kuuza kitu chochote kwenye mtandao wa Zoom Tanzania bila ya malipo yoyote. Kama haujawahi kuuza kitu mtandaoni, huu ni muda mzuri kuanza.

Kuna manufaa mengi kwa Watanzania yatokanayo na kuuza vitu vitu wasivyovihitaji. Wanaweza kupata kipato cha ziada, wanaweza kuweka huru nafasi iliyokuwa imechukuliwa na vitu wasivyovihitaji na kuitumia kwa tija zaidi, na pia wanaweza kuchochea jitihada za kulinda mazingira kwa kutokutupa vitu wasivyovitumia.

Zoom Tanzania itawapatia elimu wauzaji wake jinsi ya kuutumia mtandao wake ili waweze kusimamia matangazo yao, na kuwa uwezo wa kutangaza vitu wanavyouza pale wanapotaka. Wauzaji na wanunuzi watasaidiwa katika kila hatua ya safari hii, kupitia elimu itakayokuwa ikitolewa mtandaoni na nje ya mtandao. Pia kutakuwa na makala zitakazogusia jinsi ya kufungua akaunti, jinsi ya kuweka tangazo vizuri, jinsi ya kufanya mauzo na manunuzi salama nakadhalika. Mrejesho na maswali yanakaribishwa na wateja wanaweza kuwasiliana na timu yetu kupitia tovuti ya (www.zoomtanzania.com), kwa namba za simu, ama kupitia mitandao yetu ya kijamii.

Zoom Tanzania iko na itaendelea kuwepo, ikijizatiti kuwa mtandao wenye bidhaa tofauti na zenye ubora, na mtandao wenye usalama kutokana na njia madhubuti za uthibitisho wa vitu vinavyouzwa. Zoom Tanzania ni sehemu unayoweza kupata chochote unachotaka, popote nchini.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: