Mkuu wa Kanda ya Mashariki ya TCRA Mhandisi Lawi Odiero akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa kanda hiyo katika kijiji cha Nyandira.
Afisa wa TCRA Kanda ya Mashariki Annastella Mchomvu akiwasikiliza wananchi wa Kijiji cha Nyandira wakati kanda hiyo ilipokwenda kutoa elimu ya mawasiliano katika kijiji hicho.
Mkuu wa Kanda ya Mashariki ya Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) Mhandisi Lawi Odiero akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nyandira wakati walipokwenda kutoa elimu ya mawasiliano wa kijiji hicho
Mkuu wa Kanda ya Mashariki ya TCRA Mhandisi Lawi Odiero akitoa kitabu cha muongozo kwa mwananchi wakati wa utoaji wa elimu ya mawasiliano kwa kanda hiyo.
Wananchi wakiangalia vipepelushi mbalimbali wakati wa utoaji wa elimu kwa Kanda ya Mashariki ya TCRA
Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) Mhandisi Lawi Odiero akiwasomea wananchi juu matumizi ya mawasiliano kwa kuzingatia sheria na wataokiuka adhabu ambazo zimewekwa katika jarida hilo
Afisa wa TCRA Kanda ya Mashariki Vaolet Eseko akitoa maelezo kuhusiana na matumizi ya simu wakati kanda hiyo ilipokwenda kutoa elimu ya mawasiliano katika Kijiji cha Nyandira mkoani Morogoro.
Mkuu wa Kanda ya Mashariki ya TCRA Mhandisi Lawi Odiero na maafisa wa Kanda hiyo wakiwa katika kituo cha Radio cha Top Fm mkoani Morogoro kwa ajili ya kutoa elimu ya mawasiliano.
Wananchi wa Nyandira wakipeana maelezo mara baada ya kupata elimu ya mawasiliano kutoka Kanda ya Mashariki ya TCRA.

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
Kanda ya Mashariki ya Mamlaka ya Mawasiliano Nchini(TCRA) imeendelea kutoa elimu ya mawasiliano nchini ikiwa ni pamoja kuwataka wananchi wasajili namba zao kwa kutumia alama za vidole.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nyandira mkoani Morogoro Mkuu wa Kanda ya Mashariki ya Mamlaka hiyo Mhandisi Lawi Odiero amesema kuwa serikali imeshatangaza wananchi juu ya usajili wa namba za simu kwa alama za vidole hivyo ni vyema wasajili kwani baada ya muda uliowekwa ukimalizika namba za simu zisizosajiliwa zitafungwa na watoa huduma.

Odiero amesema kuwa usajili huo ni usalama kwa mtumiaji wa mawasiliano ambapo kwa alama hizo hawawezi kuingiliana na mtu mwingine yeyote duniani.

Amesema kuwa wananchi watumie mawasiliano kwa mujibu wa sheria zilizopo bila na mtu atakaye kwenda kinyume na sheria zilizowekwa anaweza kufungwa jela au faini na wakati mwingine ni faini pamoja na kifungo kwa wakati mmoja.

Odiero amewasaa wananchi wa Nyandira kutumia simu kwa kutengeneza ajira kwani mawasiliano yanarahisha kufanya biashara na kuweza kujiingizia kipato.

Aidha amesema kuwa kitambulisho kinachotakiwa ni cha uraia /kitambulisho cha Taifa na serikali imetoa vitambulisho hivyo na inaendelea kutoa kwa wale wasiokuwa navyo wafuatilie mamlaka husika na kuweza kuwa navyo na hatimaye kujisajili namba za simu kwa alama za vidole.

Hata hivyo amesema kuwa mtu anaweza kuwa na laini moja au zaidi isipokuwa hawezi mtu kumiliki laini mbili kwa mtandao mmoja. 

"Tumejipanga kuhakikisha wananchi wetu tunawafikia popote mlipo ili kuwapa elimu ya mawasiliano msiweze kupata changamoto katika kutumia mawasiliano hayo"amesema Odiero.

Katika utoaji wa elimu kwa wananchi kanda hiyo pia inatoa elimu kupitia vituo radio pamoja na Luninga ili kwa wale wasiweza kufika katika mihadhara hiyo kupata taarifa katika vyombo vya habari.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: