Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga Godwin Gondwe ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mhe. Godwin Gondwe akifurahia baada ya kuvalishwa medali mara alipomaliza mbio KM 21 za Tanga City Marathon 2019 iliyofanyika na kumalizikia Uwanja wa Mkwakwani. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga Godwin Gondwe ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mhe. Godwin Gondwe akimaliza Mbio za KM 21 katika Uwanja wa Mkwakwani-Tanga.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga Godwin Gondwe ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mhe. Godwin Gondwe akihojiwa na mwanahabari mara baada ya kumaliza mbio KM 21 za Tanga City Marathon zilizomalizikia Uwanja wa Mkwakwani.
Wakimbiaji wakionyesha umahili wao.

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG, Tanga.

KAIMU Mkuu wa Mkoa wa Tanga Godwin Gondwe amesema mkoa huo utaendelea kutumia mashindano ya riadha ya Tanga City Marathon kuweza kutangaza fursa za uwekezaji na utalii zilizopo mkoani Tanga.

Gondwe ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Handeni ameyasema hayo leo wakati akifunga mashindano ya Tanga City Marathon yaliyofanyika jijini Tanga ambapo msimu huu yameshirikisha washiriki 1,300 kutoka mikoa mbalimbali na nje ya nchi.

Amesema watafanya hivyo kutokana na kwamba mkoa huo kuwa na maeneo makubwa ya uwekezaji yaliyopo mkoani Tanga ili kuweza kuwa vutia kuwekeza kutokana na fursa kubwa zilizopo.

“Ndugu zangu tutaendelea kuitumia Tanga City marathon kuweza kutangaza mkoa wa Tanga... Lakini pia kutangaza utalii hata uwekezaji mkoa wa Tanga kwani tuna fursa nyingi sana ambazo mnaweza kuzichangamkia kwenye kufanya uwekezaji “ Amesema.

Hata hivyo aliwapongeza washiriki ambao wamefanya vizuri kwenye mashindano hayo na kuwataka kuendelea kujiweka imara kwa kushiriki kwenye mazoezi mara kwa mara ili kuweza kujiandaa na yale yajayo.

“Mashindano hayo ya Tanga City Marathon yameufanya mkoa wetu uweze kuendelea kutangazika lakini niwaambie waandaaji wafungue mapema dirisha la usajili msimu ujao “Alisema.

Amesema kwani iwapo watafungua mapema dirisha la usajili wanaweza kupata wadhamini ambao wataweza kuongeza chachu kwenye mashindano hayo msimu ujao.

“Pia niwaambie kwamba Mkuu wetu wa Mkoa Martine Shigella anatambua anatambua sana mchango wenu mlijitokeza kushiriki mashindano hayo na sio kwenye michezo pekee anathamini Tanga City Marathon lakini kubwa amenielezea amefurahi kusikia vijana wa shule zetu wameshiriki nao Tanga City Marathon”Amesema.

Hata hivyo pia aliwaagiza wakuu wa shule za Sekondari, Msingi na Vyuo vikuu kuhakikisha wanajiandaa kikamilifu ili kuweza kujipanga kwa ajili ya mashindano yajayo ili nao waweze kupeleka washiriki ambao watashindano kwenye mbio za kilomita tano.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: