Sehemu ya washiriki wa warsha ya siku moja iliyolenga kutathimini mustakabali wa juhudi za ukombozi wa mwanamke nchini kuelekea miaka 25 ya mkutano wa Beijing hapo mwakani.
Mwenyekiti wa TGNP Mama Assen Muro akitoa rai kwa wadau wote kuhakikisha wanatafuta ufumbuzi wa changamoto zinazosimama kama vikwazo ili wanawake waweze kupiga hatua katika kufikia maendeleo endelevu. Mwenyekiti wa TGNP Mama Assen Muro akimueleza jambo Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia walemavu, Mhe. Stella Ikupa alipowasili kwenye warsha hiyo.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia walemavu, Mhe. Stella Ikupa akizungumza na washiriki wa warsha hiyo ambapo aliwahimiza kutorudi nyuma katika jitihada za kutetea haki na nafasi ya mwanamke katika jamii.

Na Mwandishi Wetu.

Ikiwa ni wiki ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo kilele ni tarehe 8 ya mwezi Machi kila mwaka,wadau mbali mbali wamekutana jijini Dodoma kujadili na kutathimini mustakabali wa juhudi za ukombozi wa mwanamke nchini kuelekea miaka 25 ya mkutano wa Beijing hapo mwakani.

Warsha hiyo siku moja ambao iliyowakutanisha washiriki zaidi ya 100 kutoka kote nchini wakiwemo wadau mbalimbali likiwajumuisha wanawake wakiwakilisha makundi mbalimbali,wabunge,madiwani,wanasheria,waandishi wa habari pamoja na wanafunzi wa vyuo na sekondari,iliandaliwa na TGNP Mtandao kwa kushirikiana na TAWLA, Landesa, Msichana Initiative, Haki Ardhi, Haki Elimu, Care International na TAMWA.

Mkutano huo wa Beijing uliofanyika mwaka 1995 ulilenga kuwashirikisha na kuwawezesha wanawake katika maendeleo ili kuimarisha mapambano dhidi ya umaskini na hiyo yote ni kwa wanawake kushiriki katika shughuli za kimaendeleo.

Katika kuhakikisha kila mshiriki anachangia mawazo,ilitumika njia ya kuwagawa katika makundi na kujadili maana,uelewa,umuhimu,mitizamo pamoja na changamoto la azimio la Beijing katika jamii na nchi kiujumla ambapo miongoni mwa hoja zilizoibuliwa katika kuboresha jitihada za kuleta usawa wa kijinsia ni pamoja na elimu juu ya azimio bado inahitajika sambamba na ushirikishwaji wa jamii yote kwa ujumla sambamba na kueleza faida ya usawa wa kijinsia kuanzia ngazi ya familia ili kutengeneza kizazi chenye kuelewa manufaa yake.

Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yanasimamiwa na kauli mbiu inayosema “Badili fikra kufikia usawa wa kijinsia kwa maendeleo endelevu”.
Wawakilishi wa wanawake wa jamii ya wafugaji wilayani Mvomero wakiongozwa na mwenyekiti wa umoja huo Bi. Mariam Simango (wakwanza kushoto) wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri katika warsha hiyo.
Akifafanua lengo la warsha hiyo, Mary Ndaro kutoka Care International aliwaambia washiriki kwamba warsha hii ni fursa kwa wanawake kurejea azimio la Beijing imefanikiwa kwa kiasi gani na kujua ni zipi jitihada za kuongeza ili kuendelea kuikwamua hali ya mwanawake katika jamii . Kundi liliojumuisha wanafunzi katika ngazi zote pamoja na vijana likiwa makini kujadili mitazamo na uelewa juu ya azimio la Beijing ambapo kufikia 2020 litatimiza miaka 25 ya maazimio. Akichangia wakati wa majadiliano ya katika makundi,mbunge wa Mtera Mhe.Livingstone Lusinde alisisitiza kuwa azimio la Beijing halina azma ya kuwafukuza wanaume kutoka nafasi zao katika jamii, bali ni juu ya kuinua wanawake kwa hali ya juu ili waweze kupata haki zao kama wanaume na kufanya kazi pamoja kwa maendeleo ya nchi. Anna Marwa kutoka Pelum Tanzania akichangia jambo wakati wa majadiliano ya makundi yaliyolenga kupima umuhimu,mitazamo na uelewa juu ya azimio la Beijing miongoni mwa washiriki wa warsha hiyo. Zawadi Kondo mwanafunzi kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam akiwasilisha majibu kwa niaba ya kundi lililojumuisha wanafunzi katika ngazi zote pamoja na vijana.
Washiriki wakifuatilia kwa karibu mawasilisho.
Mdau wa masuala ya wanawake ambaye pia ni mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi Rachel Chibwete akiwasilisha majibu kwa niaba ya kundi lililojumuisha wabunge,madiwani pamoja na waandishi wa habari. Wanafunzi kutoka shule ya sekondari Manchali iliyopo Chamwino jijini Dodoma wakicheza kuashiria furaha yao kutokana na fursa ya kushiriki katika warsha hiyo. 
Washiriki wakishikana mikono kama ishara ya umoja na mshikamano ambayo kwa pamoja waliafiki kuwa ni nguzo muhimu katika kufanikiwa kuitetea nafasi ya mwanamke katika jamii.
Sehemu ya washiriki wakipata picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia walemavu, Mhe. Stella Ikupa 
Waandaaji nao hawakuwa nyuma kupata kumbukumbu na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia walemavu, Mhe. Stella Ikupa .
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: