Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mhe. Jokate Mwegelo (Kulia) akigawa vifaa vya shule ikiwa ni sehemu ya kampeni ya Tokomeza Zero Kisarawe - Pwani.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mhe. Jokate Mwegelo akizungumza siku alipozindua kampeni ya Tokomeza Zero katika wilaya ya Kisarawe ikiwa na lengo la kuongeza ufaulu kwa wanafunzi.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mhe. Jokate Mwegelo (wa pili kutoka kushoto) akipata maelekezo katika moja ya mahabara wilayani Kisarawe
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mhe. Jokate Mwigelo akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi katika mahafali ya kidato cha nne.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mhe. Jokate Mwegelo akifurahia jambo na wanafunzi wa shule ya Makurunge, Bagamoyo.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mhe. Jokate Mwegelo akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi katika mahafali ya Darasa la Saba.
Kila kona ni furaha...

TOKOMEZA ZERO kisarawe ni kampeni maalum kwa ajili ya kuongeza ufaulu na kuondoa kabisa Zero wilaya ya Kisarawe mkoa wa Pwani.

Tunaelewa kuwa changamoto wanazopitia waalimu na wanafunzi ni nyingi sana tunaelewa kuwa Elimu ndio ufunguo wa maisha hivyo sisi wana-Kisarawe tuukaona ni yema sana kuwekeza katika Elimmu.

Mheshmiwa mkuu wa wilaya ya Kisarawe anasema ukimsaidia mtoto akaweza kupata elimu unakuwa umeweza kusaidia Tanzania nzima na mimi kuanzia sasa nataka tuanze na kidato cha nne na sita tufute hizo ZERO na zisiwepo kabisa. Katika kuhakikisha hii linatimia kuna mambo mengi ambayo tutafanya kwa kushirikiana na wadau wote wa elimu nchini.

Mwaka jana tulifanya kammpeni hii na kukusanya wanafunzi wa kidato cha Nne na tukaweza kuongeza ufaulu wilayani, mwaka 2017 Kisarawe kulikuwa na kampeni ya ondoa Zero ambayo ilifanikiwa kupunguza zero toka 455 mpka 259 kwa kidato cha nne na kuondoa zero kabisa kwa kidato cha sita , Kwa kuona hili Mhesimiwa mkuu wa Wilaya ya Kisarawe alizindua Kampeni dada ijulikanayo kama Tokomeza Zero Kisarawe ikijumuisha wanafunzi kuwekwa kwenye kambi kwa ajili ya Massive Training uboreshwaji wa miundo mbinu mashuleni na pia Elimu na kozi kwa waalimu ili kuinua kiwango cha Elimu wilaya ya Kisarawe

Tuna lengo la kuongeza idadi ya vijana wanaongia vyuo vya kati na vikuu, 

Tunachohitaji:

Utafiti unaonyesha wanafunzi wengi wa Kisarawe hutembea umbali mrefu sana kwenda shule (Zaidi ya km 15 kwenda pekee) hali inayofanya wanafunzi kufika shuleni wakiwa wamechoka, hebu fikiri mtoto wa kike ambaye atahitajika kufanya usafi nyumbani kisha aende shule kwa kutembea huyu atachoka zaidi.

Miundo mbinu ya shule zetu ni changamoto sana n ahata Idadi za shule Wilayan ni chache ,tuna shule chache na kwa kulitambua hilo sisi tutashirikiana na wadau wa Elimu ili kuwezesha ujenzi wa shule kwa ajili ya wana kisarawe

Kwa sasa tunaweka mkazo Zaidi katika yafuatayo ili kufanikisha kampen yetu hii ya TOKOMEZA ZERO

Wanafunzi wote wa kisarawe wa kidato cha nne na cha sita watapata mafunzo ya ziada ili kujiandaa na mitihani yao ya taifa, ili kuwaepusha na kazi za kila mara wanafunzi hawa watakuwa kwenye kambi maaum kwa muda miezi miwili kabla ya muda wa mitihani yao ya taifa.

Tunawapatia waalimu mahitaji yote muimu ili kufanikisha zoezi lao la ufundishaji na pia kuboresha miundo mbinu ya shule ili kuweza kukidhi mahitaji ya wanafunzi na walimu

Tunachofanya sasa hivi:

Katika kuhakikisha tunafanikisha hili tumeandaa Dinner Gala tarehe 30/03/2019 katika jitihada za kukusanya fedha ambazo zitatumika katika ujenzi ya Bwei, shule hii itakuwa na madarasa ya kutosha, maktaba pamoja na maabara zakisasa kabisa. Shule hii itakuwa ya kwanza ya aina yake kisarawe na wewe Mdau wa Elimu unaweza kushiriki kwa kuchangia 100,000 moja au kununua meza moja kwa shilling million moja.

Hela zote hizi zitaelekezwa katika ujenzi wa shule hii ya kwanza ya aina yake yenye lengo la kuwa shule ya mfano ambapo shule zitakazofuatia zitaundwa kwa huu.

Unaweza kushiriki kwa kuwasiliana nasi kwa namba hii ili kupata ticket yako 0677062070 au 0656132676
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: