Mgeni Rasmi ambaye ni Afisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Shinyanga, Glory Mbia akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya kutengeneza Batiki kwa vikundi vya wazazi kutoka kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga yaliyoendeshwa na SIDO kwa ufadhili wa Shirika lisilo la Kiserikali The Voice of Marginalized Community (TVMC). Kushoto ni Meneja wa SIDO mkoa wa Shinyanga,Hopeness Elia,kulia ni Mkurugenzi wa TVMC,Musa Ngangala. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali The Voice of Marginalized Community (TVMC),Musa Ngangala akielezea lengo la kutoa mafunzo ya utengenezaji batiki kwa vikundi vya wazazi katika kata ya Chamaguha.
Meneja wa SIDO mkoa wa Shinyanga,Hopeness akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya kutengeneza batiki kwa vikundi vya wazazi kata ya Chamaguha katika manispaa ya Shinyanga.
Kushoto ni Meneja wa SIDO mkoa wa Shinyanga,Hopeness na Afisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Shinyanga,Glory Mbia wakiwa wameshikilia batiki iliyotengenezwa na vikundi vya wazazi kutoka kata ya Chamaguha wakati wa uzinduzi wa batiki za kwanza kutengenezwa kata ya Chamaguha kupitia TVMC.Kulia ni Mkurugenzi wa TVMC ,Musa Ngangala akifurahia batiki ya ukweli.
Uzinduzi wa batiki za kwanza kutengenezwa kata ya Chamaguha kupitia TVMC ukiendelea.
Uzinduzi wa batiki za kwanza kutengenezwa kata ya Chamaguha kupitia TVMC.Pichani ni miongoni mwa batiki zilizotengenezwa na wajasiriamali kutoka Chamaguha.
Zoezi la utoaji vyeti kushiriki na kufuzu mafunzo ya utengenezaji batiki likiendelea.
Utoaji vyeti ukiendelea.
Washiriki wa mafunzo hayo wakitengeneza batiki.
Utengenezaji batiki ukiendelea.
Zoezi la kuchanganya rangi likiendelea.
Batiki ikitolewa kwenye rangi.
Picha ya pamoja washiriki wa mafunzo ya utengenezaji batiki.
Picha ya pamoja.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog.
Shirika lisilo la Kiserikali The Voice of Marginalized Community (TVMC) Shinyanga kwa kushirikiana na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo SIDO limeendesha mafunzo ye kutengeneza Batiki kwa vikundi vya wazazi kutoka kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga.
Mafunzo hayo ya siku nne yalianza Machi 21 na kumalizika Machi 25,2019 katika ukumbi wa SIDO mkoa wa Shinyanga kwa kukutanisha washiriki 25 yakiwa na lengo la kuwakwamua kiuchumi,kuondokana na umaskini ili kuzuia mimba na ndoa za utotoni sambamba na kuanzisha viwanda vidogo vidogo.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo,Mgeni Rasmi ambaye ni Afisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Shinyanga,Glory Mbia alilipongeza shirika la TVMC kumsaidia Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli kutengeneza viwanda.
“TVMC mmeonesha kwa vitendo kuwa mnaunga mkono serikali ya Viwanda,tunawapongeza kwa kufanya kazi nzuri inayofuata matakwa ya serikali,tunaamini kuwa kupitia mafunzo haya,tutapata viwanda vidogo kutoka wajasiamali hawa na tunafurahi mmetoa mafunzo kwa kushirikiana na SIDO”,alieleza Mbia.
Aidha alisema serikali itaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo katika kuwainua kiuchumi wananchi huku akiwataka wajasiriamali kuomba mikopo kwenye halmashauri za wilaya ili kuendeleza shughuli zao.
Kwa Upande wake,Mkurugenzi wa Shirika la TVMC, Musa Ngangala alisema mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Kuzuia Mimba na Ndoa za Utotoni unaotekelezwa na TVMC kwa ufadhili wa shirika la Firelight Foundation la nchini Marekani.
“Ili kufanikisha mradi huu,mwaka 2016 tulianzisha vikundi vya ujasiriamali kwa wazazi ili kuhakikisha tunawakwamua kiuchumi ili kuondokana na umaskini ambao huchangia kwa kiasi kikubwa mimba na ndoa za utotoni,na kwa muda wa siku nne tumetoa mafunzo ya kutengeneza batiki”,alieleza Ngangala.
“Ili kuunga mkono kwa vitendo sera ya serikali ya Viwanda kupitia kwa Rais wetu Mpendwa Dkt. John Pombe Magufuli,Tunatarajia kuanzisha vyumba maalum kwa ajili ya shughuli ya utengenezaji batiki na tutatoa vitendea kazi vya kuanzia ili kuhakikisha vikundi hivi vinakuwa vya mfano katika Manispaa ya Shinyanga lakini mkoa kwa ujumla”,alisema Ngangala.
Hata hivyo Ngangala alisema TVMC itaendelea kutoa mafunzo ya aina mbalimbali ili kuwapa ujuzi wananchi wafanye shughuli za ujasiriamali ikiwa ni katika kuwaletea maendeleo wananchi.
Mara baada ya mafunzo ya Utengenezaji Batiki kumalizika,umefanyika uzinduzi wa batiki za kwanza kutengenezwa kata ya Chamaguha kupitia TVMC.
Toa Maoni Yako:
0 comments: