Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Geita mkoani Geita akipewa maelezo na Meneja wa Misitu wa wilaya wa Wakala wa Huduma ya Misitu Tanzania (TFS) Fedy Ndandika wakati alipotembelea eneo la Manga lililokuwa limevamiwa na wakulima ambayo ni moja ya eneo la Msitu wa Hifadhi Geita
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akizungumza na  wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika kata ya Mgusu, Halmashauri ya  wilaya ya Geita mkoani Geita akiwasisitiza wananchi umuhimu wakufuata  sheria na kuacha tabia ya kuvamia Hifadhi za Misitu.
Mkazi wa kata ya Mgusu, Anaeli Mbokile akizungumza mbele ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiwasilisha ombi la kumegewa eneo la Hifadhi ya Msitu Geita ili liweze kutumika kwa ajili ya
malisho na makazi baada ya wakazi wa kata ya Mgusu idadi ya kuongezeka.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiteta
jambo na baadhi ya wanachama wa CCM wakati alipomaliza mkutano wa
hadhara katika kata ya Mgusu mkoani Geita. 
(PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA).


NA LUSUNGU HELELA-GEITA


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu amewaonya  wananchi wanaofanya shughuli za kibinadamu ndani ya Hifadhi za Misitu
nchini kuacha tabia ya kuwashambulia Watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wanapokuwa wanatekeleza majukumu yao.

Onyo hili linakuja ikiwa zaidi ya watumishi watano wa TFS katika mikoa ya  Pwani, Tabora ,Kigoma pamoja Kilimanjaro wakiwa wamepoteza maisha yao kwa kushambuliwa na wananchi wakati wakiwa wanatekeleza majukumu yao.

Aidha, Mhe. Kanyasu amepiga marufuku kwa watumishi wa TFS kujichukulia sheria  mkononi kwa kuwapiga wananchi wanapobainika kutenda makosa."Watumishi wa TFS hamruhusiwi kumpiga Mwananchi mnapomkamata ndani ya Hifadhi au akiwa anasafirisha mazao ya Misitu kinyume na sheria, atakayebainika sheria itachukua mkondo wake.

Ametoa onyo hilo wakati  akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Mgusu wilayani Geita mkoani Geita ikiwa ni ziara yake ya kutatua migogoro ya mipaka kwenye msitu wa Hifadhi Geita iliyopo baina ya Vijiji ambapo jumla ya hekta 4,462.95 zimefutwa kwa tangazo la Serikali.

Amesema shughuli za uhifadhi ni lazima zifanyike kwa ushirikishwaji kati ya wananchi na watumishi wa TFS." Uhasama unaozidi kujengeka kati yenu hauna tifa katika uhifadhi shirikianeni" amesisitiza.


Mhe.Kanyasu.Amewataka wananchi kuheshimu na kuzifuata sheria za uhifadhi ya Misitu nchini huku akiwataka watumishi kujiepusha na migongano kati yao na wananchi.

Katika hatua nyingine, Mhe.Kanyasu amewataka wananchi wafuate sheria kwa kulipia vibali kwa TFS pale wanapokuwa na mahitaji ya mazao ya Misitu badala ya kusubilia mpaka wakamatwe na TFS.


Mkuu wa Wilaya ya Geita, Mhe.Josephat Maganga  amemueleza Naibu Waziri huyo kuwa hali ya Misitu katika wilaya hiyo ni  mbaya kufuatia shughuli za kibinadamu zinazoendelea kufanyika Misitu  hiyo.

Hata hivyo, Mkuu huyo wa Wilaya hiyoMhe. Maganga alisema  kufuatia hali hiyo tayari Kamati ya Ulinzi na Usalama kwa kushirikiana  TFS wameshaanza kufanya doria ya kuwaondoa wafugaji na wakulima  waliovamia Hifadhi.Katika hatua nyingine, Diwani ya Kata ya Mgusu,  Pastory Lugusa amemuomba Naibu Waziri huyo kumegewa eneo la Hifadhi
kwa vile idadi ya wakazi wa kata hiyo imeongezeka hali inayopelea kukosa
maeneo kwa ajili ya malisho na Kilimo.

Kwa upande wake Meneja wa Misitu wa wilaya wa TFS, Fedy Ndandika amemuhakikishia Naibu Waziri kuwa watashirikiana na wananchi hata hivyo tayari wameanza kutoa elimu ya umuhimu wa uhifadhi kwa jamii zinazozunguka Hifadhi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: