Mwenyekiti wa Chama cha wanawake katika fani ya Utalii Tanzania (AWOTTA) Mary Kalikawe (kushoto) akiongea na wandishi wa habari ( hawapo pichani ) jijini Dar es Salaam, wakati wa mkutano wa kutangaza Maonyesho ya biashara ya Utalii wa Ndani ya Kwanza nchini yatakayofanyika katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa Posta Dar es Salaam, Februari 15 hadi 17 ,2019. ” Kauli mbiu ya maonyesho hayo ni Tambua Ushindi wa Kibishara katika Utalii wa Ndani Tanzania” Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa TTB ,Geofrey Tengeneza na Mwenyekiti wa chama cha wanawake Tanzania katika biashara (Tanzania Women Chamber of Commerce) Jacqueline Maleko.
Mwenyekiti wa Chama cha wanawake katika fani ya Utalii Tanzania (AWOTTA) Mary Kalikawe (kushoto) Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Bodi ya Utalii Tanzania ( TTB) ,Geofrey Tengeneza (katikati) na Mwenyekiti wa chama cha wanawake Tanzania katika biashara (Tanzania Women Chamber of Commerce) Jacqueline Maleko, wakiwa wameshikana mikono kuonyesha ushirikiano wao kwa wandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wakati wa mkutano wa kutangaza Maonyesho ya biashara ya Utalii wa Ndani ya Kwanza nchini yatakayofanyika katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa Posta Dar es Salaam, Februari 15 hadi 17 ,2019.” Kauli mbiu ya maonyesho hayo ni Tambua Ushindi wa Kibishara katika Utalii wa Ndani Tanzania.
---
Chama cha Wanawake katika fani ya Utalii Tanzania (AWOTTA) kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii (MNRT), Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Chama cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC), Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) na shirika la maendeleo la Ujerumani GIZ, wameandaa documentary ambayo imeziduliwa leo jijini Dar es Salaam.

Hafla ya uzinduzi wa documentary hiyo ambayo inahusu tukio la maonyesho maonesho ya Utalii wa ndani UWANDAE EXPO 2019 yatakayofanyika mwezi ujao mwezi wa Februari tarehe 15 hadi 17 katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa (National Museum –Posta). ilifanyika katika katika ofisi za Bodi ya Utalii Tanzania na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya utalii na waandishi wa habari.

Akiongea kuhusu maonyesho haya ambayo yanafanyika nchini kwa mara ya kwanza, Mwenyekiti wa AWOTTA, ambayo inaratibu maonyesho hayo, Mary Kalikawe, alisema AWOTTA na washirika wake waamua kutekeleza mpango mkakati wa Bodi ya Utalii wa kuutangaza utalii wa ndani kwa vitendo kupitia UWANDAE EXPO 2019 na kauli mbiu ya maonyesho haya ni “Tambua ushindani wa Kibiashara katika Utalii wa Ndani Tanzania”.

“Kuzindua kwa documentary hii ikisisitiza mchango wa akina mama “Nani kama mama” kunaenda sambamba na kuzindua matangazo kwa umma wa Tanzania juu ya uwepo wa sekta kubwa ya utalii humu nchini ambayo ni muhimu ikatambuliwa kusudi ihudumiwe na kupewa umuhimu wake. Sekta hii inachochea uwekezaji kwa wingi kama tunavyoona mahoteli, usafirishaji tangu wa ndege hadi wa bodaboda, biashara ya chakula kila pembe ya nchi, burudani na utalii wa aina nyingine nyingi. Sambamba na uwekezaji huu, sekta ina uwezo mkubwa wa kutengeneza ajira kwa wakubwa na wadogo pia inabeba uwezo mkubwa wa kutengeneza kipato kwa mtu mmoja mmoja, makundi na kuchangia kipato cha taifa kwa kiasi kikubwa. Kwa sasa utalii wa mbuga za wanyama unachangia asilimia 17 ya pato zima la taifa ambayo ni takribani dola Bilioni 2.1 au shillingi zaidi ya trillion 4.7 kila mwaka”. alisema Kalikawe.

Maonesho haya yanatarajiwa kufunguliwa rasmi na Mhe. Dr. Hamisi Kigwangala, Waziri wa Maliasili na Utalii siku ya Ijumaa tarehe, 15 Februari 2019.

Lengo la Maonyesho haya ni kuanzisha utambuaji wa mapana ya sekta ya Utalii wa ndani na fursa kubwa za uwekezaji na ajira zinazoambatana na kukua kwa sekta hii muhimu. Maonyesho yatawaunganisha wafanyabiashara wa bidhaa na huduma katika maeneo mbali mbali yanayosababisaha safari za watanzania. Wafanya biashara hawa na vyombo vinavyowezesha uwekezaji, watatumia jukwaa hili kukuza uhusiano baina ya washiriki na Watembeleaji wa maonesho. Watu elfu tatu wanategemewa kuhudhuria maonyesho.

Taarifa ya tovuti https://www.nbs.go.tz/nbs/takwimu/Br/2014_15_SBR.pdf inaonesha takwimu zifuatazo: Kuwa mwaka 2014 jumla ya vitengo rasmi vya chakula vinywaji na malazi wakati huo Tanzania bara vilikuwa 11,136. Kati ya hivi asilimia 51.7 vilikuwa vya chakula na vinywaji wakati asilimia 48.3 vilikuwa ni sehemu za watu kulala.

Kwa upande wa sanaa na burudani, jumla ya vitengo rasmi katika utafiti wa mwaka 2014/15 vilikuwa 239 ambayo ni chini ya asilimia 1 ya vitengo vyote vya biashara vilivyotambuliwa mwaka huo. Kati ya hivi ubunifu na burudani vilikuwa asilimia 35.6, michezo na starehe vilikuwa asilimia 24.3, michezo ya kubahatisha na kubeti ilikuwa asilimia 23.8 na vitengo vya library, kujisomea, makumbusho na burudani za utamaduni ilikuwa asilimia 16.3

Waandaaji wa maonesho wanapenda kutangaza kuwa kupitia uelewa wa upana wa sekta zilizomo katika utalii wa ndani, takwimu hizo hapo juu zimekwishaanza kubadilika na kupanda na mwamko wa watanzania na watoa huduma katika kuboresha utalii wa ndani utapandisha sana ukuaji wa vitengo hivi vya biashara.

Ni muhimu mikoa yote itambue umuhimu wa kuvuta wageni wa ndani kwenda kutembea kwa sababu mbali mbali katika mikoa yao. Kuwasili kwa wageni ndio ukuaji wa sekta ya utalii wa ndani. Takwimu hizo hapo juu zitajidhihirisha katika mikoa mbali mbali ikifanya bidii kuvuta wageni wa ndani na kuwapa huduma nzuri kama vile wanataka wageni wasahau kurudi kwao!

Faida ya kushiriki:

-Kuonyesha bidhaa au huduma wanazozalisha au wanazotoa;

-Kupata fursa ya kujifunza teknonolija mpya na ujuzi kutoka kwa washirikiwengine;

-Kupata fursa ya kushiriki katika kongamano na semina ya bure itakayofanyika sambamba na maonyesho hayo;

-Kukutana na Wafanyabiashara, Wawekezaji, washauri wa kibiashara na Wasambazaji wa huduma mbalimbali;

-Kupata kutangazwa kwenye utandawazi wa kitaifa na kimataifa kwa njia mbalimbali;

-Kupata fursa mbali mbali ambazo ni pamoja na tiketi ya raffle, vocha ya malazi, zawadi za kusafiri n.k.

Aidha, ni fursa ya kimkakati ya kuwahamasisha wananchi wa Tanzania kupenda kutumia huduma zinazotolewa na wadau wa sekta ya utalii hapa nchini.

Maonyesho haya yanatarajiwa kushirikisha, Wizara, Taasisi, Makampuni pamoja na Wafanyabiashara wa sekta mbalimbali. Kongamano litakuwa juu ya "Biashara, Uwekezaji na Ajira katika Utalii wa Ndani ambalo litatolewa bure (idadi ni watu 250 tu kwa siku moja wataruhusiwa, hivyo jiandikishe mapema kabla nafasi hazijaisha).

Kiingilio kwenye maonesho ni bure asubuhi hadi saa 10 jioni. Kisha yanafuata masaa ya burudani ambayo inalipiwa kiasi kidogo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: