Na Ripota Wetu, Morogoro.

KATIBU wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa morogoro, Shaka Hamdu Shaka amesema Watanzania hawana shauku wala ndoto ya kufanya mabadiliko ya utawala kwa kuwategemea wanasiasa wenye mtazamo na mawazo duni.

Amesema katika kipindi hiki ambacho Serikali ya CCM ikijibadili kimfumo na kisera kukidhi matakwa ya wananchi na wakati ni vigumu vyama vya upinzani kushika dola.

Shaka alitoa kauli hiyo wakati aliposhiriki mahafali ya kwanza ya Shule ya Sekondari Morogoro Open School, Mkoani hapa. “Tofauti ya kati ya viongozi CCM na wa vyama vingine, viongozi wa Serikali ya CCM hujikuta katika kujadili hoja na utekelezaji wa mipango na si kuishi kwa nadharia isiyo na tija.

Aliongeza: “Serikali ya CCM itabaki kuamini katika siasa ya ujamaa na kujitegemea. Tangu zama za sera za uchumi hodhi na ujio wa soko huria na utandawazi, CCM imekataa kushikilia ukale bali hufanya mabadiliko ya kisera,”alisema

Alisema anayefikiria siasa ya ujamaa na kujitegemea imekufa hawana uelewa kwani serikali inaposomesha wanafunzi bure, kutoa huduma bora za afya ni katika utekelezaji wa msingi ya ujamaa. Katibu huyo wa CCM mkoa, alisema wanasiasa hawapaswi kukosoa kwa pupa na jazba badala yake wawe na vipimo vya uhalisia wa madai yao kwani wananchi ni werevu, wanajua kutofautisha yaliyokuwepo na ufanisi wa mabadiliko yanayooneka.

Shaka aliwahimiza wanafunzi kuendelea kujenga matumaini kwa sera za CCM kwani ndicho chama chenye uwezo wa kufanyakazi kwa uhodari katika kuleta maendeleo. “Nawawatia
shime wanafunzi mjipe jukumu la kusoma kwa bidii. Wale waliohitimu watambue wana jukumu la kujiandaa mwa kutumia fursa zinazotolewa na serikali pia mshiriki ushindanikwenye soko la ajira” alisema Shaka.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: