Mmoja wa wateja waliotembelea katika duka la Danube la GSM Group, lililopo Mlimani City jijini Dar es Salaam, Miss Tanzania 2005,Nancy Sumari(katikati) akionyeshwa baadhi ya biddhaa zinazouzwa dukani hapo kwa BEI CHEE na Afisa Mauzo wa Duka hilo,Habiba Said maduka hayo yameanzisha kampeni ya”BEI CHEE” yenye lengo la punguzo la bei kwa asilimia 70% ili kuwanufaisha wateja wake hususani msimu huu wa maandalizi ya sikukuu kwa bidhaa mbalimbali katika maduka yote yaliyopo katika Mall ya Mlimani City na Pugu,Kushoto ni Meneja Uendeshaji wa maduka hayo yaliyopo chini ya GSM Group,Haji Mfikirwa.
Afisa Mauzo wa Duka la Danube la GSM Group lililop Mlimani city jijini Dar es Salaam, Habiba Said (kushoto)akimuonyesha moja ya chombo cha kuwekea matunda,Miss Tanzania 2005,Nancy Sumari (kulia)ambaye alitembelea duka hilo kununua vitu mbalimbali, Maduka hayo yameanzisha kampeni ya”BEI CHEE” yenye lengo la punguzo la bei kwa asilimia 70% ili kuwanufaisha wateja wake hususani msimu huu wa maandalizi ya sikukuu katika maduka yote yaliyopo katika Mall ya Mlimani City na Pugu.Katikati ni Meneja Uendeshaji wa maduka hayo yaliyopo chini ya GSM Group,Haji Mfikirwa.
---
*Sasa punguzo ni kwa asilimia 70%

Siku chache baada ya GSM Tanzania kuzindua kampeni ya “BEI CHEE” yenye lengo la punguzo la bei kwa asilimia 70% ili kuwanufaisha wateja wake hususani msimu huu wa maandalizi ya sikukuu kwa kununua bidhaa mbalimbali katika maduka yao ya DANUBE yaliyopo katika Mall ya Mlimani City na Pugu,Wananchi wengi ambao tayari wameanza kunufaika na kampeni hiyo jijini Dar es Salaam wamesema kampeni hii ni silaha ya kuondoa umaskini kwenye familia nyingi na ikitumiwa ipasavyo itapendezesha nyumba zao na wengi kuwanunulia zawadi wanaoishi nje ya Dar es Salaam.

Wakiongea kwa nyakati tofauti baada ya kutembelea duka la Danube lililopo jijini Dares Salaam mlimani city, baadhi ya wateja wamesema kuwa endapo wananchi wengi wenye vipato vya chini au vya juu wataichangamkia kampeni hii wengi wao ndoto zao za kumiliki bidhaa nzuri zenye kupendezesha manyumbani kwao au maofisini zitatimia.

“Mmoja wa wateja akiongea na waandishi wa habari katika duka hilo lililopo mlimani city jijini Dar es Salaam kuhusiana na Kampeni hiyo Nancy Sumari ambaye alikuwa Miss Tanzania 2005 ambaye kwa sasa anajishughulisha na shughuli zake za ujasiriamali alisema kama ambavyo tumeelekezwa ni kampeni ya kipee kabisa ambayo haijawahi kutolewa hapa nchini kwa ajili ya kutunufaisha sisi tukiwa kama wateja wa maduka haya”,Alisema

Aliongeza kuwa kwa jinsi alivyopata tu habari kupitia njia ya mtandao alifunga safari yake kuja kununua bidhaa mbalimbali kwani hakutegemea kabisa katika maisha yake kama angekuja kusikia Danube ina kampeni ya aina hii kwani bidhaa zao zinauzwa kwa bei chee kabisa na ndiyo maana ameacha kazi zake zote za ujasiliamali na kuja kununua

bidhaa hizo na amegundua kuwa Danube ni mkombozi kwa wajasiriamali nchini na ametoa wito kwa watanzania kuichangamkia frusa hiyo,Alisema Sumari

Akiongelea kampeni hii inayoendelea,Meneja Uendeshaji wa maduka ya Danube Tanzania yaliyopo chini ya GSM Group,Haji Mfikirwa amesema kuwa kampeni ya“BEI CHEE”imelenga kuwanufaisha wateja wa GSM na wananchi kwa ujumla nchi nzima na kwa jinsi gani wanaweza kunufaika na msimu huu wa maandalizi ya sikukuu ili wapate kufurahia na familia zao kwani wamesikia kilio chao na kuamua kuwaletea bei chee.

“Tunafurahi kuona wateja wetu wameipokea kampeni hii vizuri kwa kuona hivi tunafarijika sana na tunapenda kutoa wito kwa wale wote ambao awajapata nafasi ya kutembelea maduka yetu watembelee ili waje kunufaike na bidhaa zetu nyingi zenye bei chee kabisa, kwani kampeni kama hizi zinafanyika mara chache sana kwa mwaka na hii ndiyo frusa ya kipekee”.Alisema Mfikirwa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: