MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia akizungumza kuhusiana na maonyesho hayo kushoto ni Mhasibu wa SIDO mkoani Tanga Janeth Kiwale.
Afisa Uendelezaji Biashara (SIDO) Mkoa Tanga Gladness Foya akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maonyesho hayo ambayo yatafanyika katika viwanja vya Tangamano Jijini Tanga kesho na kushirikisha Nchi toka Jumuiya ya Afrika Mashariki kulia ni Mhasibu wa SIDO Mkoani Tanga Janeth Kiwale
ZAIDI ya wajasiriamali 250 wamekwisha wasili Jijini Tanga kwa ajili ya maonyesho ya Shirika la kuhudumia viwanda vidogovidogo (SIDO) Kanda ya Kaskazini yanayotarajiwa kuanza kesho Nov 22 hadi 26 ambapo mgeni anatarajiwa kuwa Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Joseph Kakunda
Hayo yamezungumzwa na Afisa Uendelezaji Biashara (SIDO) Mkoa Tanga Gladness Foya alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maonyesho hayo ambayo yatafanyika katika viwanja vya tangamano Jijini hapa na kushirikisha Nchi toka Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Foya alisema maandalizi yapo vizuri na tayari baadhi ya wafanyabaishara toka Nchini Uganga na Burundi wamekwisha wasili kwa ajili ya maonyesho hayo ambayo yanajumuisha mikoa ya Tanga,Kilimanjaro.Arusha na Manyara.
“Tumekwisha anza pokea wageni na wapo zaidi ya wajasiriamali 250 wamekwisha wasili na watatu toka Uganda na watano toka Burundi na tunatarajia kupokea
wageni zaidi katika maonyesho haya”Alisema Foya.
Awali akizungumzia maonyesho hayo Mkuu wa Mkoa Tanga Martin Shigella alisema ni fursa kwa Watanzania na wananchi wa ndani ya jiji na nje kujifunza namna Serikali ya awamu ya tano inavyotekeleza kwa vitendo uchumi wa viwanda.
Aidha alisema tayari taasisi za kifedha,wamili wa viwanda na wasindikaji wamekwisha wasili Jijini hapa kwa ajili ya maonyeshoi hayo ambayo yatawajenga katika nyanja hiyo ya uchumi wa viwanda na ujasiriamali.
“Tunaowageni wengi tumekwisha anza wapokea na zaidi ni fursa kwetu na wajasiriamali maana watapata muda wa kuuza bishara zao na kuona bidhaa zinazozalishwa na sido na wanaweza kuomba kutengenezewa labda niseme tu ni fursa kubwa” Alisema Shigella.
Hata hivyo aliwaomba wafanya biashara kuyatumia maonyesho hayo ili kuweza kujinufaisha kibiashara na namna ya kuweza kupata bidhaa bora toka shirika hilo la Sido.
Toa Maoni Yako:
0 comments: