Mkurugenzi Mkuu wa Biko, Charles Mgeta wa pili kutoka kulia akimkabidhi hundi ya sh milioni 20 na nyumba iliyopo Kigamboni mshindi wao Prisca Msuya wa katikati aliyeibuka kidedea kwenye droo kubwa iliyochezwa juzi Jumatano. Wengine ni Afisa Leseni wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Catherine Lamwai kushoto akifuatiwa na Kajala Masanja Balozi wa Biko pamoja na Meneja Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Tuntufye Mwambusi. Picha na Mpigapicha Wetu.
Mkurugenzi Mkuu wa Biko, Charles Mgeta akimkabidhi hundi ya sh milioni 20 na nyumba iliyopo Kigamboni mshindi wao Prisca Msuya aliyeibuka kidedea kwenye droo kubwa iliyochezwa juzi Jumatano. Picha na Mpigapicha Wetu. Mshindi wa nyumba alia kwa uchungu kufuatia ushindi wa biko
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
Mshindi wa nyumba na sh milioni 20 wa Biko, Prisca Msuya wa Mbezi jijini Dar es Salaam, amelia kwa uchungu mbele ya waandishi wa habari wakati anakabidbiwa hundi ya ushindi wake wa fedha na nyumba kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) iliyopo Kigamboni, huku akishuhudiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Biko, Charles Mgeta.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari, mama huyo ambaye ni mjasiriamali mdogo wa duka, alisema kitu kinachomliza ni kushinda nyumba na sh milioni 20 kutoka Biko, huku akitokea kwenye maisha duni ya kuishi kwenye chumba na sebule.
"Siamini macho yangu kwamba kweli nimeshinda nyumba kutoka Biko, maana maisha yangu ya nyuma anayajua Mungu, ingawa tangu Biko inaanza nilikuwa namuomba Mungu ili niweze kushinda zawadi za juu ikiwamo sh milioni 10, jambo ambalo Mungu amenitimizia mara mia moja.
"Kwakweli namshukuru sana Mungu kwa zawadi hii pamoja na kuwaombea Biko katika mtazamo wao wa kuleta utajiri kwa watu wake, hivyo Watanzania wote naomba tucheze Biko kwa sababu ndio michezo halali unaoweza kutoa mamilioni pamoja na nyumba,"Alisema.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Biko, Charles Mgeta, alisema mchezo wao umeanzishwa kwa lengo moja la kuwakwamua Watanzania, wakiwamo wadau wa kubahatisha, akisema kila mtu anapoibuka na ushindi anazunguukwa na watu wanaotumia ushindi huo kuboresha maisha yao kwa pamoja.
"Leo hii tunamkabidhi dada Prisca fedha na nyumba, ila tunaamini wapo watoto wake, mume na ndugu ambao kwa namna moja ama nyingine watakuwa wamekwamuliwa na mchezo wetu wa Biko.
"Tunaomba Watanzania wote waendelee kucheza Biko ili wapate nafasi ya kushinda zawadi zetu maana kucheza ni rahisi ambapo namba ya Kampuni ni 505050 na kumbukumbu ni 2456, huku wanaocheza sana ndio wenye nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi kutoka kwetu Biko,"Alisema.
Akizungumzia mchezo wa Biko, Afisa wa Leseni wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Catherine Lamwai, alisema Biko ni mchezo halali unaofuata sheria, kanuni na taratibu zote, huku akisema uwapo wake una manufaa makubwa kwa jamii pamoja na serikali kwa ujumla.
"Mtu yoyote anayeshinda Biko lazima kuna sehemu yake ya ushindi inaenda kwa serikali kama kodi, huku Biko nao kama Kampuni wakikatwa kodi hivyo kuchangia kwenye pato la Taifa, hivyo Watanzania waendelee kucheza ili wapate ushindi,"Alisema.
Naye Meneja Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Tuntufye Mwambusi, alisema mshindi wa Biko hajapata nyumba tu, ila nyumba bora inayofaa kukaliwa na binadamu wenye ndoto kama Prisca.
"Hii ni fursa adhimu ambayo imeenda kwa mshindi wa Biko, ambapo ameshinda nyumba kutoka Biko, huku tukipewa fursa pana ya kutoa nyumba zetu kama NHC kwenda kwa washindi jambo ambalo ni la kizalendo linalofanywa na watu wa Biko, hivyo kwa niaba ya menejimenti ya NHC nafikisha pongezi kwao huku nikiwataka Watanzania wote wacheze Biko bila kuchoka ili washinde fedha na nyumba kwa ajili ya kubadilisha maisha yao," Alisema.
Bahati Nasibu ya Biko ni mchezo unaotoa nafasi kubwa ya ushindi ambapo mbali na kushinda nyumba, pia zawadi za papo kwa hapo zinaendelea kutolewa kuanzia sh 5000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na sh 1,000,000 huku Jumapili hii zawadi ya mamilioni au nyumba zikitarajiwa kwenda kwa washindi katika droo kubwa ya Jumapili hii.
Toa Maoni Yako:
0 comments: