Bw. Andrew Mwalwisi, Mkurugenzi Msaidizi, Elimu Ushirikishwaji wa Wafanyakazi kutoka Idara ya Kazi akitoa mafunzo kwa wajumbe wa baraza kuhusu majukumu na wajibu wao.
Sehemu ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi wakifuatilia kwa makini mafunzo ya utekelezaji wa majukumu ya baraza.
Bi. Rukia Adam, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Bima akitoa hotuba ya uzinduzi wa Baraza la wafanyakazi.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima wakiimba kwa pamoja wimbo wa "Solidarity Forever" kuashiria umoja wa wafanyakazi.
---
Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima Nchini imezindua baraza la pili la wafanyakazi ili kusimamia utendaji na utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka hiyo kama ilivyoainishwa katika Mpango Mkakati wa miaka mitano.
Baraza hilo limezinduliwa leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Fedha na Mipango baada ya baraza la kwanza la kuisha muda wake.
Akiongea katika uzinduzi wa baraza hilo Bi. Rukia Adam ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Bima amewataka wajumbe wa baraza hili watambue majukumu yao katika kipindi chote cha miaka mitatu na pia wawe na uwezo wa kufikiri zaidi ili kukuza na kuendeleza soko la bima nchini.
“Dhamana mliopewa na wafanyakazi wenzenu ni kubwa na muhimu sana kwani mnatakiwa kusimama kama kiungo muhimu cha kutoa dira ya utekelezaji wa malengo ya Mamlaka kwa mujibu wa Mpango Mkakati wake” alisema Bi. Rukia.
Katika kuendeleza soko la bima nchini, baraza hili linapaswa kuhakikisha menejimenti na wafanyakazi wote kwa pamoja wanaimarisha taswira na muonekano wa huduma za bima nchini, kukuza uwezo wa kitaaluma na kimtaji miongoni mwa makampuni ya ndani na watendaji wake, kukuza mchango wa sekta ya bima katika ajira na pato la taifa, na kuwafikia wananchi wengi hususan wenye kipato cha chini.
Kwa upande wake Bw. Andrew Mwalwisi, Mkurugenzi Msaidizi, Elimu na Ushirikishwaji wa Wafanyakazi kutoka Idara ya Kazi alitoa mafunzo ya wajibu wa wajumbe wa baraza kwa Menejimenti ya Mamlaka na kwa wafanyakazi wenzao.
“Ieleweke kuwa mjumbe wa baraza la wafanyakazi kikanuni ana majukumu manne ambayo ni kushauri kuhusu mwenendo na utendaji wa Mamlaka, kurekebisha, kukosoa kwa nia njema na kushukuru utendaji wa uongozi, alisema Bw. Mwalwisi.
Akieleza matarajio ya Mamlaka kwa Baraza hili Dkt. Baghayo Abdallah Saqware ambaye ni Kamishna wa Bima na Mwenyekiti wa Baraza, amesema kuwa mabaraza ya wafanyakazi ni vyombo muhimu katika ustawi wa taasisi yeyote. Hivyo, anatarajia baraza hili litakuwa na machango chanya kwa taasisi kama lilivyokuwa baraza lililopita.
Toa Maoni Yako:
0 comments: