Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akizindua mradi mkubwa wa maji wa uboreshaji wa huduma ya maji mjini Mbinga uliogharimu Sh. Bilioni 1.029 akiwa na DC Mbinga, Cosmas Nshenye.
Sehemu ya mradi wa maji wa uboreshaji wa huduma ya maji mjini Mbinga.
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akifungua maji katika mradi wa maji Kagugu, wilayani Mbinga katika mkoa wa Ruvuma kuashiria kukamilika kwake.
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akicheza ngoma katika hafla ya kusheherekea kukamilika kwa mradi wa maji Kagugu, wilayani Mbinga, mkoani Ruvuma.
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akiwa juu ya tenki la mradi wa Mkako, wilayani Mbinga, mkoani Ruvuma.
Sehemu ya watu waliohudhuria hafla ya kusheherekea kukamilika kwa mradi wa maji wa Kagugu, wilayani Mbinga, mkoani Ruvuma.
---
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa amezindua mradi mkubwa wa uboreshaji wa huduma ya maji mjini Mbinga akiwa katika ziara yake kikazi mkoani Ruvuma.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Profesa Mbarawa amesema mradi huo ni hatua ya Serikali kufikia lengo la kufikia asilimia 90 kwa miji mikuu ya wilaya itakapofika mwaka 2020, na imepanga kutumia Silingi Bilioni 1.2 kwa ajili ya kuboresha huduma ya maji kwa miji mingine 25 Tanzania Bara na Visiwani.
Amesema mradi huo utabadilisha kwa kiasi kikubwa maisha ya wananchi wa Mbinga sio tu kwa kutoa huduma ya majisafi na majitaka kwa wananchi. Pia, ni muhimu kwa shughuli za kila siku za kiuchumi zinazofanyika katika mji huo.
Vilevile, Profesa Mbarawa ameipongeza Mamlaka ya Maji ya Songea Mjini (SOUWASA) kwa kazi nzuri ya kusimamia mradi huo mpaka umekamilika.
Mradi huu upo chini ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira ya mji wa Mbinga (MBIUWASA) ulianza kujengwa Mei, 2017 chini ya mkandarasi Almasi General Supplies Ltd ya Songea na kuanza kutoa huduma ya maji kwa mji wa Mbinga Februari, 2018 umegharimu Shilingi Bilioni 1.029.
Naye Meneja wa MBIUWASA, Patrick Ndunguru amesema kukamilika kwa mradi kumeleta ongezeko la uzalishaji wa maji kutoa wastani wa lita 700,000 wakati wa kiangazi na lita 1,600,000 wakati wa masika, ikichangia kuongeza mapato kutoka Shilingi Milioni 18 hadi Milioni 25 kwa mamlaka hiyo.
Wizara ya Maji kwa kutumia Kampuni ya Don Consult ilisanifu mradi huu kwa lengo la kumaliza tatizo la maji katika mji wa Mbinga, pamoja na mfumo wa uondoaji salama wa majitaka.
Toa Maoni Yako:
0 comments: