Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru akimkabidhi cheti Katibu Muhtasi wa Mamlaka ya Bandari Zanzibar, Bi. Zainabu Abdallah baada ya mkurugenzi huyo kuhitimisha mafunzo ya siku tatu jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa ukimwi.
Mmoja wa makatibu muhtasi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara mkoani Morogoro, Bi. Farida Mfaume akipokea cheti cha ushiriki baada ya kuhitimishwa kwa mafunzo leo.
Katibu Muhtasi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), Neema Makuluni akipokea cheti cha ushiriki kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Museru.
Baadhi ya washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo leo ambayo yamefanyika kwa siku tatu kwenye hospitali hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Prof. Museru akiwa katika picha ya pamoja na washiriki baada ya kufunga mafunzo hayo leo.
---
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imehitimisha leo mafunzo ya elimu ya jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa ukimwi kwa makatibu muhtasi kutoka mikoa mbalimbali nchini na kuwatunuku vyeti vya ushiriki.

Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Muhimbili kwa kushirikiana na Chama cha Makatibu Muktasi Tanzania (TAPSEA) yaliyodumu kwa muda wa siku tatu ambapo wametarajiwa kuisambaza elimu hiyo kwa watu wengine ili wafahamu namna ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi.

Akizungumza kabla ya kuwatunuku vyeti makatibu muktasi hao, Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Prof. Lawrence Museru amesema wameweza kutekeleza moja ya azma ya hospitali ya na sera ya serikali ya kutoa elimu ili makatibu muktasi waweze kujikinga na ugonjwa huo.

“Naomba elimu hii iwe endelevu na mkawe mabalozi wazuri katika kuonyesha manufaa ya mlichojifunza hata kwa wale ambao mtawakuta katika maeneo yetu ya kazi na jamii kwa ujumla,” amesema Prof. Museru.

Alitumia nafasi hiyo pia kuwaeleza kuwa hospitali inajipanga kuandaa mafunzo mengine ambayo yatazungumzia mada mbalimbali kulingana na jinsi makatibu muktasi watakavyopendekeza ili kuwasaidia katika maeneo yao ya kazi pamoja na katika maisha yao kila siku.

Aidha Prof. Museru ametoa rai kwa jamii kuwa wazi pindi mtu anapogundulika kuwa ameathirika na ugonjwa wa ukimwi na kuanza kuchukua hatua za haraka ili kuweza kupata matibabu kwa wakati ili kujikinga na kuwakinga wengine.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: