By Proff.
Jana usiku ndugu Hubert Mufuruki alituma kwenye group la 'THE UPCOMING HEROES' orodha ya mambo 9 ya kusaidia kiusalama kwa Wanasiasa, wanaharakati au wafanyabiashara wakubwa. Nilipoyasoma nimeongezea mengine 16 na hivyo kufanya jumla kuwa 25. Ni mambo yatakayokusaidia kwa ajili ya usalama wako hasa kama wewe ni Mwanasiasa, Mwanaharakati, au Mfanyabiashara mkubwa;
1. Usimuamini SANA mtu mwingine hasa asiye ndugu yako. Hata kama ni rafiki inabidi uwe na 'limit'katika kumuamini. Kwa maisha ya sasa pesa ina nguvu kuliko kitu chochote. Kwa ushawishi wa pesa mtu yeyote aweza kuuza ramani ya wewe kukamatwa kwa kutumia advantage ya urakifi wenu.
2. Usijulikane ratiba yako ya kutoka na kurudi nyumbani. Yani ukiwepo na usipokuwepo watu wasione tofauti kubwa. Pia kama una gari usizoee kutoka na gari siku zote. Siku nyingine panda bodaboda, au daladala, na hata kutembea kwa miguu. Kama una gari zaidi ya moja, jifunze kubadili gari. Usiendeshe hiyohiyo kila siku hadi watu wakariri. Kama unarudi nyumbani usiku usiwe na njia moja ya kurudia.
3. Usipende kutabirika katika baadhi ya mambo kama vile chakula au kinywaji ukipendacho. The only person to know your "favourite dish" ni mkeo/mumeo. Leo ukikutana na marafiki ukala kuku choma, kesho kula chips mayai, next time usile kabisa. Mtu akijua chakula ukipendacho ni rahisi kukudhuru. Kama ni kinywaji do as much as possible kunywa chochote ili mradi hakikupi shida. Leo kunywa juice, kesho beer, next time maji. Sio kila siku unakunywa kinywaji kimoja, kiasi kwamba wenzio wanaweza kukuagizia kabla hata hujafika. Hii ni hatari.!
4. Usipende sana kula au kunywa kwa mtu ambaye hujamzoea sana. Umekutana na mtu mara ya kwanza au ya pili unaagiza chakula/kinywaji. Don't dare. Kama una njaa hakikisha umekula kwanza kabla ya kukutana nae.
5. Kama umeacha kinywaji nusu ukaenda 'washroom' ukirudi usitumie kilichobaki. Agiza kingine. Na usipende sana kutumia glass kwa mtu ambaye hujamzoea.
6. Usipende kumaliza kinywaji unapojitayarisha kuondoka mahali popote. Ondoka ukiwa umeacha sehemu ya kinywaji mezani. Mtu akijua unataka kuondoka na unamalizia kinywaji anaweza kukuwekea chochote katika kinywaji chako ukadhurike mbele ya safari.
7. Usipende sana kuweka picha wala taarifa za familia yako kwenye mitandao (watoto, mke, mume, wazazi etc). Pia usipende kuweka wazi taarifa zao nyingine kama vile anapofanya kazi mumeo/mkeo, au aina ya biashara anayofanya. Strangers wanaweza kumdhuru mwanao, mwenzi wako au mzazi wako ili kukufanya upunguze nguvu ya harakati. Pia wanaweza kumharibia mumeo/mkeo anapofanyia kazi au kuhujumu biashara zake ili uwe busy kujipanga kimaisha upunguze nguvu kwenye harakati.
8. Maisha yako binafsi yabaki kuwa ya kwako. Don't put in public mahali unapoishi, aina ya gari unayoendesha (wala namba zake), idadi ya watoto ulionao etc. Pia usipende sana kupiga picha kwenye mazingira ya nyumbani kwako (iwe nje au ndani). Usiwakaribishe watu usiowafahamu vizuri nyumbani kwako. Hii mambo ya kukutana na mtu kwenye group la whatsapp kesho anataka kuja kwako, itakuja kukucost.
9. Hakikisha namba yako ya simu inayojulikana na watu wengi haipo kwenye smart phone ili kuepuka kuwa tracked. We hujiulizi kwanini watu wengi siku hizi wana simu za vitochi? Namba yako iliyo public weka kwenye kitochi, kwenye smart phone weka namba unayowasiliana na watu maalumu tu, hasa familia yako.
10. Usipende kuwasha 'location' kwenye simu yako. Ukizima 'location' kama mtu anakutrack ataona mnara unaotumia (CL site) lakini hatajua hasa uko wapi. Yani kwa mfano umezima location mtu anayekutrack ataoneshwa simu yako inatumia mnara wa Muhimbili. Kwahiyo atakuja mpaka Muhimbili lakini hatajua upo exactly sehemu gani. Kwahiyo ili akupate inabidi azunguke zunguke maeneo yote ya Muhimbili. Lakini kama umewasha 'location' akikutrack ataoneshwa mpaka wodi uliyopo.
11. Ukipigiwa simu ukaulizwa upo wapi (hata kama ni mzazi wako) danganya uwepo wako. Kama upo Dar sema upo Bagamoyo. Kama upo Moshi sema uko Usa river. Danganya location yako hata kwa umbali wa kilomita 100. Hii itawachanganya wanaokufuatilia, maana wataona CL site inasoma tofauti na maelezo yako.
12. Tengeneza "code language" kisha share na mtu unayemuamini. Mnaweza kuwa na kikundi chenu kwa ajili ya kupeana taarifa kwa codes. Kwa mfano 'D3' maana yake unafuatiliwa, 'S4' means upo kwenye hatari, 'EL5' means upo kwenye hatari kubwa zaidi. Hii itasaidia kuwapa wenzio taarifa kirahisi pale unapojihisi haupo salama. Kumbuka watekaji hawakupi muda wa kutosha kupiga simu au kutuma sms na kuanza kutoa maelezo marefu. Kwahiyo ni vizuri uwasiliane kwa codes. Ukishajihisi upo kwenye hatari piga simu taja code husika then kata. Uliyempigia atajua upo kwenye hatari ataanza kusambaza taarifa za kukusaidia.
13. Usipende sana kutembea peke yako hasa nyakati za usiku. Kama mnakunywa mahali hakikisha kuna mtu uko nae utakayekwenda nae mpaka nyumbani kwako. Otherwise ondoka mapema.
14. Kama huwa unatumia bodaboda, Bajaj au Ubber usiwe na mtu 'specific' wa kukubeba. Anaweza kutumika kukudhuru. Jifunze kubadilisha. Leo ukipanda hii, kesho nyingine. Usijenge mazoea na yeyote.
15. Badilisha simu yako ya smartphone kila baada ya miezi mitatu. Itasaidia kubadili IMEI namba yako.
16. Hakikisha namba yako ya whatsapp ukipigiwa haipatikani. Na kama itabidi kupatikana basi iweke kwenye simu ya tochi. Otherwise unaweza kusajili namba hata nje ya nchi ukawa unaitumia whatsapp lakini ukipigiwa haipatikani. Hii ina manufaa sana kiusalama.
17. Usipende sana kutuma sms za kawaida au kupiga simu kwa njia ya kawaida kwa mambo sensitive. Kumbuka sms zote unazotuma kwa njia ya kawaida zinaweza kusomwa na simu zote zinaweza kusikilizwa na kutumika kama ushahidi mahakamani (kumbuka kesi ya Lema) if the need arise. Hakuna privacy kwenye sms wala simu za kawaida. Usijiachie sana huko. Fanya mawasiliano ya kawaida kama kuwapigia wazazi na kuwasalimia, lakini si9 mambo sensitive.
18. Njia ambayo kwa sasa ni salama kupiga simu na kutuma text ni Whatsapp na Telegram, kwa sababu taarifa inatoka kwa mtumaji kwenda kwa mpokeaji moja kwa moja kwa kupitia 'domain' ambayo ipo Marekani. Hakuna mtu wa kati kuwasikiliza. Na kama kuna mtu anafuatilia taarifa zako basi inabidi aombe kwenye server Marekani, jambo ambalo si rahisi. Kwahiyo kama una issue sensitive piga whatsapp call au andika text kwa whatsapp. Privacy ni 100% guaranteed. Naposema whatsapp simaanishi kwenye magroup. Huko kwenye magroup kuna mashushushu kibao. Be careful.
19. Usipende kujiunga magroup usiyoyafahamu vizuri. Siku hizi kuna mashushushu wapo kazini, wanaanzisha magroup na kuwaingiza mkenge vijana. Mtu anaandika kwenye facebook "weka namba yako nikuadd kwenye group fulani" na wewe unaweka. Acha uzwazwa. Au anatuma link anakuambia click ujiunge kwenye group fulani na wewe unajiunga fasta. Hujui muasisi wa group ni nani, limeanzishwa kwa malengo gani, unajipeleka kichwakichwa tu. Ukiwa huko unaanza kufunguka na kujikuta matatizoni.
20. Kama wewe ni Admn wa group usiadd watu usiowajua vizuri. Unaletewa namba ya mtu humjui unaambiwa "Admn add huyo jamaa ni kamanda wetu mpiganaji yupo Kigoma" na wewe una add tu kama zwazwa, kumbe ni namba ya OCS Oysterbay.
21. Usiwaamini sana rafiki wa rafiki zako au rafiki wa ndugu zako. Mmekutana mnakunywa, halafu kesho anakupigia. Mimi fulani rafiki yake mjomba wako tulikunywa wote jana. Mnaanzisha mawawasilino, unamkaribisha nyumbani kwako. Anaomba kwenda toilet kumbe anasoma ramani ya nyumba. Be careful.
22. Ukiwa unarudi nyumbani (hasa nyakati za usiku) hakikisha geti la nyumbani liko wazi. Mpigie mlinzi afungue, kama huna mlinzi basi whoever available akufungulie kabla hujafika nyumbani. Usisubiri ufike kisha ndipo upige honi ufunguliwe. My friend utaumia.
23. Kama upo barabarani hasa nyakati za usiku kila baada ya dakika mbili angalia kama unafuatiliwa. Ukihisi kufuatiliwa ingia hata kituo cha mafuta zuga kidogo, na kama wanaokufuatilia nao wataingia au kupunguza mwendo wakusubiri utoke, jua upo kwenye hatari. Anza kujulisha watu wako wa karibu kwa code language.
24. Kama una usafiri binafsi hakikisha gari yako kila siku haipungui mafuta nusu tenki, ili hata kama unakimbizwa uwe na uwezo wa kwenda mwendo mrefu. Sio unakimbizwa kutokea Morocco unafika Magomeni mafuta yanaisha. Huo ni uzembe.
25. Kama una uwezo hakikisha unamiliki silaha na muda wote upo nayo, lakini watu wasijue kama unamiliki silaha. Hii itakusaidia unaposhambuliwa kuweza kujihami, na kujiokoa katika baadhi ya situations. Usikubali kutekwa kirahisi.
Toa Maoni Yako:
0 comments: