Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro afanyia kazi Maelekezo ya kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa 2018 ambapo katika ziara ya Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Meru Wilayani Arumeru kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Ndugu Charles Francis Kabeho mbali nakukubali kuzindua barabara ya UbungoNdoombo Alitoa maelekezo kwa Mkuu wa wilaya ya Arumeru kuhakikisha mkandarasi anafanya marekebisho Madogomadogo yaliyobainika wakati wa zoezi la ukaguzi wa barabara hiyo kabla ya kuzinduliwa na Mwenge wa Uhuru kitaifa 2018.
Kutokana na sababu hizo ilimlazimu Dc Muro kukesha na kupambana kumsimamia mkandarasi huyo Pamoja na TARURA Halmashauri ya Meru na kuhakikisha marekebisho hayo yamefanyika kwa kuzingatia ushauri na Maelekezo ya kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa 2018 Ndugu Charles Kabeho yanatekelezeka kwa haraka.
Dc Muro amelazimika kufanya ukaguzi wa mwisho huku akiwa ameambatana na kiongozi wa TARURA ambapo ilimlazimu na yeye kutumia futi na baadhi ya vifaa vingine ili kujiridhisha na vipimo vya barabara Pamoja na ubora wa tabaka za udongo zilizojazwa katika barabara hiyo kama ambavyo walifanya viongozi wa mbio za Uhuru kitaifa 2018.
Kwa upande wako baadhi ya wananchi waliokuwepo wakati wa zoezi la ukaguzi wa barabara hiyo wamempongeza Dc Muro kwa hatua yake ya kurudi tena katika mradi huo wa barabara na kufanya ukaguzi kama alivyoelekezwa na viongozi wa mbio za Mwenge kitaifa 2018, wananchi hao wamesema licha ya mradi huo wa barabara kuzinduliwa na mbio za Mwenge ambao ulishaondoka Wilaya ya Arumeru lakini Dc Muro ameonyesha hekima na busara kwa kuamua kurudi tena katika mradi huo na kufanyia kazi maelekezo ya viongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa ikiwa ni kielelezo cha utashi wake binafsi katika utendaji kazi.
Toa Maoni Yako:
0 comments: