Hello friend , moja kati ya kazi zangu zakila siku ni kufundisha waandishi wa habari pamoja na kushauri makampuni matumizi (bora) ya mitandao ya kijamii kwa “faida”.
Kwaleo ntaomba nigusie kwakufupi sana kuhusu (#) hashtag nawe kama unalakuongeza karibu
Hiki kialama cha hashtag # kinakufanya wewe uliyekitumia kukuunganisha na wengine duniani kote wanaotumia kialama hicho kwa neno kama lako hilo hilo. Mfano kwa sasa Tanzani tuna majonzi ya #mvnyerere basi ukibonyeza hapo itakupeleka kwenye kurasa zenye habari zote kama hii.
Sasa basi ni muhimu sana kutumia neno sahihi , herufi sahihi kama neno la kwanza ni herufi kubwa au ndogo ili na wewe uweze kuwa mmoja wao wa waliopost kuhusu jambo hilo
Watu wengi wamekuwa wakishiriki kwenye mijadala ya kitaifa , kidunia bila ya kuweka hashtag nakujikuta wakikosa fursa ya kujumuika na wengine hivyo basi kama unataka kuwa mmoja kati ya wengi hakikisha unatumia ( hashtag term) sawasawa ili ujumuike nao.
- unapoweka hashtag hakikisha hii alama #naManenoYanaungana UsiacheNafasi*
Mitandao ya kijamii inatofautiana kuna mingine inakupa option ya kuona neno linalo trend au linalotumiwa na wengi na kuna ambayo haikupi hivyo ni wewe kujua ( somo la kujua nini kina trend ni siku nyingine)
Kuna faida na hasara nyingi tuu za kutumia common hashtag hivyo mtu unatakiwa uwe na uelewa hapa hususan makampuni tofauti na wananchi wa kawaida wanaotaka kushiriki katika mazungumzo tuu.
Faida ya kutumia hashtag moja ni kuwa mtaanza ku trend katika eneo lenu kijiografia mf. Dar kisha kitaifa Tz kisha mnaweza kwenda global na hapo sasa hata haya makampuni yanayomiliki mitandao ya kijamii yanaweza kuweka kiutambulisho flani mfano google au Facebook wanawekaga flag kuashirikia kitu fulani.
( kwa wanaopost kuhusu ajali ya meli wanaweza kujaribu hii kwakutumia hashtag Insta ni #mvnyerere na Twitter ni #MVNyerere )
Nb.angalia hiyo hashtag term inatumika kwenye nini sana . Mf. Unaweza kujitungia yako kumbe huko kwingine duniani ni “tusi” na hivyo post yako ikajumuika na post za matusi.
Nakutakia matumizi bora ya mitandao ya kijamii na kwa faida.
Leah Mushi - Communication specialist & Digital Trainer
Toa Maoni Yako:
0 comments: