Habari za mda huu... Naandika kwa masikitiko makubwa sana juu ya watu wanaopenda kutumia vibaya huruma ya raisi wetu, haswa wasanii wa bongo movie.

Jamani sera ya raisi wetu ni kila mtu afanye kazi na ndiyo maana slogan yake inasema "HAPA KAZI TU" Ukifanya kazi na kujituma kama sisi mbona maisha ni mazuri tu hapa Tanzania jamani, ila ukipenda mteremko ndiyo inaweza kukugharimu.

Dada yangu Shilole, yaani juzi tu umepost bonge la jumba hapa kila mtu akafurahia na kukupongeza hadi mie nilikupongeza, japokuwa wiki moja kabla ya hapo kuna kijana alikuwa anadai pesa zake za pili pili.

Leo nimeshangaa kuona video inasambaa ukilia na kuomba rais akusaidie kukusomeshea mtoto, sitaki kukupinga ila nakuuliza na kukushauri. Jambo ambalo nakuuliza ni kwamba, Je? Umesahau kuwa elimu ni bure kuanzia chekechea hadi form four ? Je ! Huyo unayetaka someshwa yuko darasa la ngapi dada yangu?

 Mimi nadhani vitu vingine tungevipima kabla ya kuamua kuchukua hatua. Hebu jiulize, leo raisi akikulipia ada ya mwanao unadhania hawa watoto wa maskini kabisa ambao hawana hata makazi watajisikiaje kama sio kutaka kubebeshana lawama?? Mimi nadhani wasanii tutumie majina yetu kusaidia jamii isiyojiweza na sio kutafuta mteremko.

 Kweli marafiki zako wote umeshindwa hata kuwakopa kimya kimya hiyo pesa ya ada kisha uwarejeshee kidogo kidogo pale biashara inapokwenda sawa? Nadhani hichi ulichokifanya ulistahili kukifanya kwa niaba ya mtu ambaye hana jina wala connection kama zako ili utumie jina lako kumuombea msaada kwa raisi, na siyo mwanamke mpambanaji kama wewe.

Mie nadhani ungeandika andiko ambalo ungempelekea raisi na ukaomba akudhamini ili upate pesa Benki Milioni 400 au Zaidi ukakopeshwa na ukafungua hotel kubwa na pia utakua umetengeneza ajira kwa vijana wenzetu kuliko hilo wazo.

Pia kumbuka juzi tu tulikuwa na msiba kule Chato nadhani badala ya kuibuka leo na kutaka msaada angarau ungejitokeza na rambirambi kidogo ili ikuwekee mazingira mazuri ya kuja kukiwakilisha hichi kilio chako hapo baadaye. Haya ni maoni yangu kama Mtanzania huru, sitaki povu hapa jamani. Kamati yangu ya kublock kaeni mkao wa kura.kama unaweza kuzunguka na Ttcl nchi nzima na ukahamasisha na wananchi wa @ Mwamza, Mwanza, Tanzania
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: