Makamu wa Mwenyekiti wa Chama cha wanasheria wanawake (TAWLA) Bi. Lulu Ng'wanakilala akizungumza wakati akifungua mkutano wa kuimarisha uwezo wa majukwaa ya wanawake na vijana katika kujadili Changamoto zinazowakabili wanawake kushiriki kwenye shughuli za kisiasa uliofanyika kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam leo.
Makamu wa Mwenyekiti wa Chama cha wanasheria wanawake (TAWLA) Bi. Lulu Ng'wanakilala akisisitiza jambo wakati akizungumza alipofungua mkutano.
Sara Kinyaka Mwanachama wa Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA) akitoa mada katika mjadala wa mkutano huo uliofanyika katika hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam.
Isabela Nchimbi Mwanasheria wa Chama cha Wananasheria wanawake (TAWLA) akifafanua jambo wakati akichangia hoja katika mkutano uliofanyika kwenye Hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam
Josephine Arnold Afisa Mradi TAWLA akifafanua jambo wakati akitoa ratiba ya mkutano huo.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada katika majadiliano hayo.
Sara Kinyaka Mwanachama wa Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA) akifurahia jambo wakati akitoa mada katika mjadala huo uliofanyika katika hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam
Makamu wa Mwenyekiti wa Chama cha wanasheria wanawake (TAWLA) Bi. Lulu Ng'wanakilala amesema TAWLA inatekeleza mradi wenye kuongeza ushiriki wa wawakilishi wanawake na vijana katika shughuli za kisiasa na Uongozi katika serikali na Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ikiwa ni pamoja na ngazi za serikali za mitaa na vijiji.
Ngw'anakilala ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa kuimarisha uwezo wa majukwaa ya wanawake na vijana katika kujadili Changamoto zinazowakabili wanawake katika kushiriki kwenye shughuli za kisiasa uliofanyika kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam.
Amesema lengo la mkutano huo ilikuwa kujengeana na kuimarisha majukumu na kujadili Changamoto zinazowafanya wanawake washindwe kushiriki kikamilifu kwenye shughuli za kiuongozi na siasa.
"Nataka wanawake tuliomo katika mkutano huu tukishajadiliana tutoe mapendekezo namna ya kuainisha na kutatua changamoto ili kumwezesha mwanamke kushiriki kikamilifu katika shughuli za kisiasa na kupata fursa ya kuwa kiongozi katika serikali na Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.
Mkutano huo ulijumuisha majukwaa ya wanawake katika ngazi mbalimbali wakiwemo wabunge, Madiwani na wale waliowahi kugombea ubunge na udiwani kutoka vyama vya siasa vya CCM, CHADEMA, CUF na ACT Wazalendo
Toa Maoni Yako:
0 comments: