MKUU wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa kulia akiwa na Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani wakimsubiri Waziri wa Uvuvi na Mifugo Mh. Luhaga Mpina kufanya nae kikao ikiwa ni mpango mkakati wa kufanikisha changamoto na utekelezaji wa ubunifu katika sekta ya uvuvi inayoongoza kwa mapato na kutegemewa na wakazi wengi wa Pangani kulia ni Afisa Tawala wa wilaya ya Pangani Gipson
Waziri wa Uvuvi na Mifugo Mh. Luhaga Mpina kulia akimlaka Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa wakati alipofika ofisini kwake kwa mazungumzo kufanikisha changamoto na utekelezaji wa ubunifu katika sekta ya uvuvi inayoongoza kwa mapato na kutegemewa na wakazi wengi wa Pangani.
Waziri wa Uvuvi na Mifugo Mh. Luhaga Mpina akiwa na Mkuu wa wilaya ya Pangani wa pili kutoka kushoto na Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani kulia akiwa na Afisa tawala wa wilaya hiyo Gipson mara baada ya kufanya mazungumzo nao leo Jijini Dodoma

Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Pangani ikiongozwa na Mh. Zainab Abdallah kwa ushirikiano na Ofisi ya Mbunge imefanya ziara ya kikazi makao makuu ya nchi mkoani Dodoma ikiwemo kukutana na kuwa na kikao na Waziri wa Uvuvi na Mifugo Mh. Luhaga Mpina na kufanikisha changamoto na utekelezaji wa ubunifu katika sekta ya uvuvi inayoongoza kwa mapato na kutegemewa na wakazi wengi wa Pangani.

Akizungumza baada ya kikao hicho Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah alisema kikao hicho kilihusisha agenda nne kubwa muhimu kwa ukombozi wa sekta ya Uvuvi wilayani Pangani ikiwemo Upatikanaji wa mashine ya Storage (Compressor) na Jokofu kwa ajili ya kuhifadhi mazao ya baharini kwa ajili ya soko kubwa la Samaki Pangani Mashariki ambalo ujenzi wake umefanikishwa na mapato ya ndani ya halmashauri.

Hatua hiyo imepelekea Waziri Mpina kuwapongeza kwa jitihada za awali na kuahidi kuwa Wizara yake itatoa fedha ili jokofu na compressor vipatikane mara moja na soko lianze kufanya kazi.

Alisema kuelekea utekelezaji wa kampeni ya “VIJANA NI WAKATI WETU” iliofanyika Wilaya ya Pangani; sekta ya uvuvi ndio iliongoza kwa uandikishaji wa Vijana wengi.

Hivyo pia Mkuu huyo wa wilaya aliwasilisha  ombi la kupata Engine za Boti za uvuvi kwa ajili ya vikundi vya vijana walio tayari kujiajiri na kujipatia kipato kupitia sekta hii. Wizara kupitia ruzuku yake itagharamia 40% na 60% igharamie halmashauri husika.

Ambapo kufuatilia ombo hilo Wizara hiyo  imeridhia kutoa Engine za kutosha kwa vijana na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kupitia Halmashauri itatumia mfuko wa vijana na mfuko wa Jimbo kufanikisha upatikanaji wa
Engine hizi ili vijana wapate vifaa hivi vya kisasa na utaratibu utawekwa kupitia Idara ya Vijana ya wilaya juu ya usimamizi na mafunzo. Hii ni ishara ya ukombozi kwa vijana wa Pangani.

Mkuu huyo wilaya alisema pia walizungumzia suala la kuanzishwe kwa  Chuo cha mafunzo na utaalamu kwa Sekta ya Uvuvi Pangani ikiwa ni kuelekea kupata muarobaini wa sintofahamu ya Chuo cha KIM kurudi mikononi mwa wananchi na kuwanufaisha zaidi ya ilivyo sasa.

Hatua hiyo ilimlazimu Waziri huyo kuamua kuunda timu ya wataalamu ambayo itakwenda Pangani mara moja kuchunguza suala hili ili ripoti itakayo wasilishwa aweze kuitolea maamuzi kwa maslahi mapana ya wana Pangani.

Sambamba na hilo liligusiwa suala la ujenzi wa  Soko la Samaki na Dagaa Kipumbwi ambapo Waziri Mpina ameweka wazi kuwa suala hili lipo sasa kwenye mipango ya Wizara na kilichobaki ni Utekelezaji wa haraka. na ikumbukwe mipango ilishawekwa sawa juu ya urasimishaji wa Bandari ya Kipumbwi.

"Sekta ya Mifugo nayo  haikuachwa nyuma kwa Waziri kuhahidi upatikanaji wa Rambo la malisho ya mifugo Pangani ikiwa ni faraja iliopotea muda mrefu kwa wafugaji wa Pangani "Alisema.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: