Sehemu ya waokoaji wakiwa katika pembezoni mwa kivuko cha Mv. Nyerere kilichopinduka na kupelekea idadi kubwa ya watu kupoteza maisha na wengine kujerukiwa, katika eneo la Ukara, Kisiwa cha Ukerewe jijini Mwanza, wakiangalia maeneo mbalimbali kutafuta miili au watu waliohai waliozama kwenye maji. ajali ya Kivuko cha MV. Nyerere kinachofanya safari zake kati ya Bugorora na Ukara katika wilayani ya Ukerewe mkoani Mwanza kilipinduka juzi Alhamisi (Septemba 20, 2018) kikikadiriwa kubeba idadi kubwa ya abiria kuzidi uwezo wake. Kwa Mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isack Kamwelwe, Mpaka wakati huu miili ya waliopolewa majini imefikia 209, huku kati yao miili 172 imetambuliwa huku 112 ikiwa imechukulia na ndugu zao. Picha zote na Steve Magombe a.k.a Kasampaida.
---
Meli yenye vifaa maalum vya kukinyanyua na kukigeuza kivuko cha MV Nyerere kurahisisha uokoaji imewasili katika kijiji cha Bwisya Kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella ameieleza MCL Digital leo Jumapili Septemba 23, 2018 leo kuwa kazi ya kunyanyua kivuko hicho itafanywa na wataalam wa masuala ya usafirishaji na uokoaji.

Mwandishi wetu ameshuhudia baadhi ya wataalam wa uokoaji, wakiwemo wazamiaji wakishusha majini baadhi ya maboya yatakayotumika kukinyanyua kivuko hicho.

Kazi ya kukinyanyua kivuko hicho inatarajiwa kufanikisha upatikanji wa miili zaidi kutokana na kile kilichoaminika kuwa ipo miili iliyokandamizwa, kulaliwa na mizigo ndani ya kivuko.

Meli malaum ya kampuni ya Nyehunge yenye winchi la kunyanyua vitu vizito, tayari imesogezwa hatua chake na kilipozama kivuko cha MV Nyerere.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: