Katikati ni Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya bunge ya masuala ya UKIMWI, Oscar Mukasa ambaye ni mbunge wa Jimbo la Biharamulo akifungua warsha kuhusu shughuli zinazotekelezwa na Asasi ya kitaifa isiyo ya kiserikali ya Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) iliyofanyika Septemba 13,2018 katika Ukumbi wa Msekwa bungeni Dodoma Septemba 13,2018 - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog.
Mheshimiwa Oscar Mukasa akizungumza wakati wa warsha hiyo.
Mkurugenzi wa Asasi ya kitaifa isiyo ya kiserikali ya Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI), Dk. Sekela Mwakyusa akijitambulisha kwa Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya bunge ya masuala ya UKIMWI.
Dk. Sekela akiwaeleza Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya bunge ya masuala ya UKIMWI jinsi AGPAHI inavyozingatia miongozo ya Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto katika mapambano ya VVU na Ukimwi kwa kuhakikisha kuwa watoto,wanawake na familia zao kwa ujumla wanapata huduma bora za VVU na UKIMWI.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza,John Mongella akitoa ushuhuda wa kazi nzuri zinazofanywa na AGPAHI katika mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza,John Mongella alisema AGPAHI wamekuwa wadau wakubwa katika mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI mkoani Mwanza.
Wajumbe wa bodi ya AGPAHI na maafisa kutoka AGPAHI wakiwa ukumbini.
Mtoa huduma kutoka kituo cha Tiba na Matunzo katika kituo cha afya Makorola mkoani Tanga Rukia Majatta ambaye anaishi na VVU kwa miaka 28 sasa akielezea huduma zinazolewa na AGPAHI na kuwataka waliopata maambukizi ya VVU kuzingatia matumizi ya dawa za kufubaza makali ya VVU.
Kijana Edson Justin kutoka mkoani Shinyanga ambaye ni muelimisha rika kuhusu masuala ya VVU na UKIMWI akielezea huduma zinazotolewa na AGPAHI kwa watoto na vijana waliopata maambukizi ya VVU.
Mtoa huduma kutoka mkoani Simiyu,Michale Bundala ambaye anaishi na maambukizi ya VVU pamoja na mke wake akielezea kuhudu huduma zinazotolewa na AGPAHI na jinsi yeye na mkewe walivyozaa mtoto ambaye hana maambukizi ya VVU.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kahama,Underson Msumba akifafanua kuhusu huduma zinazotolewa na AGPAHI katika halmashauri yake.
Mkuu wa wilaya ya Maswa mkoani Simiyu Dk. Seif Shekalaghe akiwashukuru AGPAHI kwa jitihada wanazofanya juu ya mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga,Mheshimiwa Azza Hilal Hamad ambaye ni mjumbe wa Kamati ya kudumu ya bunge ya masuala ya UKIMWI akizungumza wakati wa warsha hiyo na kupongeza kazi zinazofanywa na AGPAHI katika kuwahudumia watanzania.
Mjumbe wa Kamati ya kudumu ya bunge ya masuala ya UKIMWI,Raphael Chegeni ambaye ni mbunge jimbo la Busega akiishukuru AGPAHI kwa kuendelea kutoa huduma za tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na maambukizi ya VVU.
Katikati ni Mbunge wa Jimbo la Kalenga, Mheshimiwa Godfrey William Mgimwa ambaye ni mjumbe wa wa Kamati ya kudumu ya bunge ya masuala ya UKIMWI akichangia hoja wakati wa warsha hiyo.
Katikati ni Mjumbe wa Kamati ya kudumu ya bunge ya masuala ya UKIMWI, Mheshimiwa Frances Mwalongo ambaye ni mbunge wa jimbo la Njombe Mjini akichangia hoja wakati wa warsha hiyo.
Mjumbe wa Kamati ya kudumu ya bunge ya masuala ya UKIMWI,Mheshimiwa Richard Ndassa ambaye ni mbunge wa Sumve akizungumza wakati wa warsha hiyo na kuomba serikali na wadau mbalimbali kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu masuala ya VVU na UKIMWI.
Mjumbe wa Kamati ya kudumu ya bunge ya masuala ya UKIMWI,Mheshimiwa Joyce Sokombi ambaye ni mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Mara akizungumza wakati wa warsha hiyo na kuipongeza AGPAHI kwa huduma inazotoa.
Picha ya pamoja washiriki wa warsha hiyo.
Picha ya pamoja maafisa wa AGPAHI na wajumbe wa Kamati ya kudumu ya bunge ya masuala ya UKIMWI.
Septemba 12,2018 katika viwanja vya Bunge Dodoma : Maafisa wa AGPAHI,Wajumbe wa bodi ya AGPAHI na wadau wa AGPAHI wakiwa katika picha ya pamoja kwenye banda la maonesho ya shughuli zinazofanywa na AGPAHI.
Katikati ni Meneja wa Huduma za Kitabibu kutoka AGPAHI, Dkt. Sarah Matemu akimwelezea mheshimiwa mbunge Philipo Mulugo (kushoto) kuhusu shughuli zinazofanywa na AGPAHI kuhusu mapambano dhidi ya VVU. Kulia ni Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Mwanza,Cecilia Yona.
Wabunge wakiwa katika banda la maonesho la AGPAHI.
Mratibu wa Tathmini na Ufuatiliaji kutoka AGPAHI, Felix Muchira akitoa ufafanuzi wa huduma zinazotolewa na AGPAHI katika vituo vya tiba na matunzo.
Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Shaurimoyo Zanzibar Mheshimiwa Mattar Ali Salum akisikiliza kwa umakini maelezo kutoka kwa Meneja wa Huduma za Kitabibu AGPAHI, Dkt. Sarah Matemu kuhusu huduma za VVU na UKIMWI zinazotolewa na AGPAHI. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog.
Toa Maoni Yako:
0 comments: