Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuonya mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko kwa kushindwa kuwasiliana na mdhamini wake na kutoa sababu za msingi mahakamani.

Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ametoa onyo hilo leo Agosti 6,2018 wakati kesi ya kufanya maandamano yasiyo halali inayowakabili viongozi 9 wa Chadema akiwemo Mwenyekiti wao Freeman Mbowe ilipokuja kwa ajili ya washtakiwa hao kusomewa maelezi ya awali.

Kabla ya kutolewa onyo hilo, wakili wa serikali Mkuu, Faraja Nchimbi ameeleza kuwa shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya washtakiwa kusomewa PH lakini mawakili wa utetezi hawakufika mahakamani.
Wakikli Hekima Masipo alidai mahakamani hapo kuwa Wakili wa washtakiwa Peter Kibatala yupo Mahakama kuu huku Jeremiah Mtobesya akiwa katika kesi nyingine Mtwara.

Hata hivyo, mahakama ilimtaka mshtakiwa wa 5, Esther Matiko ambaye hakufika mahakamani hapo tarehe iliyopita na shahidi wake akaeleza kuwa alipatwa n dharura, basi aelezee hiyo dharula yake.

Matiko amedai kuwa alipigiwa simu ya dharura kwenda shuleni anaposoma mwanaye Agosti 1, 2018 na akaondoka saa 4 usiku. Ambapo baada ya kufika shule aliambiwa mtoto wake ni mgonjwa na alipompeleka hospital alikutwa na Tetekuwanga na akaambiwa apumzike kwa siku 4.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Mashauri alimuhoji Matiko kuwa mbona mdhamini wake alishindwa kuieleza mahakama kwamba amekwenda Kenya kufanya nini.

"Nakupa warning mara nyingine uwe muwazi, hii iwe mara ya mwisho, siku nyingine unapaswa kumueleza mdhamini wako ni dharura gani imekupata," Hakimu Mashauri.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 13, 2018 kwa ajili ya washtakiwa kuja kusomewa PH.

Mbali na Mbowe, washitakiwa wengine ni Katibu mkuu wa CHADEMA, Dk. Vincent Mashinji, Mbunge wa Iringa Mjini Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu na Naibu katibu Mkuu bara na Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe Halima Mdee na    Mbunge wa Bunda, Esther Bulaya.

Miongoni mwa mashitaka  yanayomkabili washitakiwa hao ni kula njama kwa nia ya kutenda kosa, kufanya mkusanyiko usio halali, kufanya mkusanyiko wenye ghasia na kukiuka tamko la kutawanyika na kuendeleza mkusanyiko wenye ghasia.

Washitakiwa hao wanadaiwa kati ya Februari mosi na 16, mwaka huu, Dar es Salaam kwa pamoja na ujumla wao walikula njama ya kutenda makosa ya kufanya mkusanyiko usihalali, mkusanyiko wenye ghasia na kukiuka tamko la kutawanyika.

Mbowe na wenzake pia wanadaiwa Februari 16, mwaka huu, katika viwanja vya Buibui na barabara ya Mwananyamala na Kawawa, Kinondoni, wakiwa wamekusanyika kwa nia ya kutekeleza azma ya pamoja ya kuandamana hivyo kuwatia hofu wananchi kwamba kutakuwa na uvunjifu wa amani. 

Pia wanadaiwa wakiwa na wenzao 12 ambao hawapo mahakamani siku hiyo waliandamana isivyo halali wakiwa na lengo la kuvamia ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni na kutokana na mkusanyiko huo wa ghasia walisababisha kifo cha Akwilina Akwiline na majeraha kwa  askari H. 7856PC Fikiri na E6976 CPL Rahim Msangi. 
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: