Bi Stella Singano, mtoa huduma za msaada wa kisheria (Paralegal) kutoka Temeke, akitoa elimu juu ya haki za ujasiriamali kwa wakazi wa Mbagala wakati wa Tamasha la uhamasishaji lililoandaliwa na Peoples Development Forum (PDF) chini ya ufadhili wa LSF.
Kikundi cha sanaa cha Machozi kikitumia sanaa kufundisha jamii kuhusu haki za binadamu na usaidizi wa kisheria katika tamasha lililofanyika Mbagala jijini Dar es Salaam.
Katika kuwafikia wananchi na kuwaelimisha kuhusu maswala ya haki za binadamu na msaada wa kisheria , taasisi ya Peoples Development Forum(PDF) chini ya ufadhili wa Legal Services Facility imeendesha Tamasha la burdani na kutoa elimu mbagala mkoani Dar es saalam
Katika tamasha hilo elimu juu ya haki katika ujasiriamali na maswala mbalimbali ya haki na sharia ilitolewa na vilevile watoa huduma za msaada wa kisheria (paralegal) kutoka Temeke walipata fursa ya kuongea na wananchi na kuandikisha matatizo yao yanayohitaji msaada wa kisheria
LSF kwa kushirikiana na wadau wake nchi nzima imekuwa ikiwawezesha watanzania kwenye kila wilaya Tanzania bara na Zanzibar kupata msaada wa huduma za kisheria kupitia watoa huduma za msaada wa kisheria bila gharama yoyote
Kupitia mradi huu unaofadhiliwa na DANIDA na DFID , LSF imewawezesha wananchi kupata haki zao, utatuzi wa migogoro midogo midogo na msongamano mahakamani, imetoa elimu juu ya maswala mbalimbali ya kisheria na kuelimisha jamii umuhimu wa kulinda haki za binadamu, lakini pia imeshirikiana na serikali, kupitia wizara ya Katiba na Sheria, katika uandaaji na hatimaye kupitishwa kwa sheria mpya ya kutambua wasaidizi wa kisheria nchini (Legal Aid Act 2017).
Lengo kubwa la mradi huu ni kutoa huduma za msaada wa kisheria kwa jamii maskini hususani wanawake na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa kuamasisha jamii kuheshimu haki za binadamu
Toa Maoni Yako:
0 comments: