Maisha ya mwanadamu siku hizi ni maisha yaliyojaa chuki na visasi Tukiishi katika maisha ya chuki na kulipizana visasi bila kusameheana basi tutazidi kusambaratika na dunia itakua siyo sehemu salama kuishi kwa kila mmoja wetu.
Msamaha ni nini?
-Msamaha ni kuondoa uchungu wote ulioumbika ndani ya moyo wako kwa hiari yako mwenyewe.
Zifuatazo ni faida za kusamehe:-
1.Tunasamehe kwasababu kusamehe ni amri na ni agizo la Mungu Tunapaswa kusameheana kwani muasisi wa msamaha ni Mungu mwenyewe na kama Mungu angehesabu maovu yetu nani angesimama? Anza leo kusamehe, hakuna aliye mkamilifu.Hata wewe hivyo ulivyo sio Mkamilifu
2. Tunasamehe ili tuweze kusamehewa.
Unapaswa kusamehe kwa faida yako mwenyewe siyo kwa faida ya mkosaji na wewe hebu mwachie Mungu apambane na watesi wako wala usilipe kisasi.
3. Unasamehe ili uwe na amani. Unaposamehe unakuwa unapata amani ya moyo. Mtu ambaye anavumilia uchungu ulioumbika ndani ya moyo na hataki kuachilia fundo hilo lazima litamtesa na atakosa amani ya moyo. Atahangaika na huku uchungu ulioumbika ndani ya moyo ukiendelea kumtafuta.
4. Unasamehe ili uwe na furaha. Kwa kweli ukiangalia watu wanaokataa kusameheana huwa hawana furaha kabisa katika mioyo yao. Kama unaishi katika mahusiano yoyote na mara nyingi huwa watu si wakamilifu basi msamaha ndio kiunganishi chenu ambao utarudisha uhusiano uliopotea
5. Tunasamhe ili tuwe na afya njema
Uponyaji wa kweli unaanzia moyoni. Kama mtu anasamehe kutoka moyoni basi huo ni msamaha wa kweli na ni msamaha unaoongozwa na huruma ya Mungu ndani yake. Watu hawataki kusamehe ndio maana wengine afya zao ni dhaifu. Uchungu ulioumbika ndani ya moyo unaendelaa kuwatafuna. Usizeeke kabla ya wakati kwa ajili ya kutosamehe watu wengine
6. Kutosawasamehe watu kunakufanya ujikinai wewe mwenyewe.
Unajiona wewe ni mtu ambaye hustahili kuwepo hapa duniani. Utajiona wewe hauna maana hapa duniani utakua unakaa peke yako peke yako.
Huna furaha, amani, upendo. Maisha yako yanakuwa yamejaa sumu na majeraha moyoni ugonjwa umekuwa mkubwa na wewe hutaki kuupatia dawa ya kuuponya na dawa yake ni msamaha tu.
🙌BADILIKA SASA 🙌
Toa Maoni Yako:
0 comments: