Mwezeshaji katika mafunzo ya msaada na huduma za kisaikolojia, Dk. Joseph Musagasa akielezea umuhimu wa kupima afya kabla ya kuanzisha mahusiano ya kimapenzi au kuingia katika ndoa.
Dk. Musagasa akizungumza wakati wa mafunzo hayo. Aliwataka watu wanaoishi na maambukizi ya VVU kuzingatia matumizi sahihi ya dawa zinazofubaza makali ya VVU pamoja na kuzingatia lishe bora.
Chausiku Sita kutoka kituo cha afya na matunzo cha hospitali ya Ngudu halmashauri ya wilaya ya Kwimba akielezea namna vijana wanavyopata maambukizi ya VVU kutokana na kukosa elimu sahihi kuhusu VVU na Ukimwi. Alisisitiza umuhimu wa kuwa muwazi unapobainika kuwa una maambukizi ya VVU.
Musa Ordas kutoka kituo cha afya Nyehunge kilichopo katika halmashauri ya wilaya ya Buchosa akichangia hoja wakati wa mafunzo hayo.
Mhudumu wa afya kituo cha afya Sengabuye iliyopo katika halmashauri ya manispaa ya Ilemela, Bahati Balekele Boyi.
Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Mwanza, Cecilia Yona akielezea faida za kuzingatia lishe bora kwamba inasaidia kuwa na afya njema.
Washiriki wakijifunza kwa njia ya picha.
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa ukumbini.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog.
Toa Maoni Yako:
0 comments: