Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mhandisi Mwanasha Tumbo wa tatu kutoka kulia akiwa na Mbunge wa Jimbo la Muheza Balozi Adadi Rajabu wa pili kutoka kulia wakipokea mifuko 600 ya saruji kutoka kwa kampuni ya Lucky Cement ya Kisarawe Mkoani Pwani kwa ajili ya kuanza ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Muheza kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Muheza,Like Gugu.
Mkuu wa wilaya ya Muheza ,Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kupokea saruji hiyo ambapo aliishurku kampuni hiyo huku akiyataka makampuni mengine yaliyopo mkoani hapa kuunga mkono jitihada hizo kulia ni Mbunge wa Jimbo la Muheza,Balozi Adadi Rajabu kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Muheza, Like Gugu
Mbunge wa Jimbo la Muheza, Balozi Adadi Rajabu akizungumza katika halfa hiyo ambapo aliishukuru kampuni hiyo kwa kuamua kuwasaidia ujenzi huo huku akiyataka makampuni mengine kuiga mfano huo.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Lucky Cement iliyopo Kisarawe,Emanuel Muya akizungumza na waandishi wa habari kuhusu azma yao ya kusaidia mifuko ya saruji 600 kwa ajili ya ujenzi wa Hospital ya wilaya ya Muheza kushoto ni Mkuu wa wilaya hiyo,Mhandisi Mwanasha Tumbo kulia ni Mbunge wa Jimbo la Muheza,Balozi Adadi Rajabu na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Muheza,Like Gugu
---
MKUU wa wilaya ya Muheza, Mhandisi Mwanasha Tumbo, Mbunge wa Jimbo hilo, Balozi Adadi Rajab na wakazi wa wilaya hiyo wakishirikiana kwa pamoja wameanza kuchimba msingi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya katika Kijiji cha Lusanga Kata ya Lusanga ambayo itasaidia kuondoa changamoto ya kutokuwepo kwa kipindi cha miaka 37.

Hatua ya viongozi hao ina lengo la kuandika historia tokea wilaya hiyo ilipoanzishwa mwaka 1974 ambapo wananchi walikuwa wakitegemea kupata huduma za matibabu kwenye hospitali ya Teule Muheza kutoka maeneo mbalimbali kabla ya kufikiria kuanzishwa kwa hospitali hiyo ambayo itakayogharimu zaidi ya bilioni 11.

Akizungumza wakati akishiriki zoezi la uchimbaji wa mtaro wa Hospitali hiyo na kupokea mifuko ya saruji 600 ya Lucky kutoka kwa Kampuni ya kuzalisha Saruji ya Kisarawe, Mhandisi Mwanasha alisema waliamua kufanya hivyo kutokana na kuwepo kwa changamoto ya huduma ya afya ambayo ilimlazimu wakati ameteuliwa kuiongozi wilaya hiyo kukutana na wadau kuweza kuona namna ya kuweka mikakati ya kupatikana kwake.

Aidha kutokana na kuwepo kwa hospitali ya wilaya walikuwa wakilazimika kutimia hospitali ya teule Muheza tokea ilipoanzishwa lakini imeonekana kuzidiwa na watu wanaohitaji huduma hasa ukizingatia pia zahanati na vituo vya afya vipo vichache huku wananchi wakiongezeka.

“Nilibaini changamoto ya hospitali ya wilaya wakati nilipokuwa nikifanya vikao kwa kuzunguka kata zote nikaona tatizo la huduma ya afya ni kubwa sana na hivyo kuonekana kuna haja ya ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Muheza lakini hata kwenye baraza la madiwani suala hilo lilizungumzwa”Alisema.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: