Mbunge wa Mufindi Kaskazini Mahamoud Mgimwa akiwa kwenye moja ya darasa ambalo litakarabatiwa kutumia mfuko wake wa jimbo ili liwe kwenye kiwango kinachotakiwa
Mbunge wa Mufindi Kaskazini Mahamoud Mgimwa akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua majengo ya shule na kuangalia majengo yapi yanastahili kukarabatiwa
Mbunge wa Mufindi Kaskazini Mahamoud Mgimwa akiwa kwenye moja ya zahati ambayo inatakiwa kufanyiwa ukarabati ili kuboresha huduma za afya kwa wananchi wa kata ya Mapanda

Na Fredy Mgunda, Mufindi.

Mbunge wa Mufindi Kaskazini Mahamoud Mgimwa amekabidhi jumla ya mifuko ya saruji 400 na bati 150 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa madarasa ya shule za msingi pamoja na zahati za Kata ya Mapanda kwa lengo la kuboresha maendeleo ya wananchi wa jimbo hilo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, alisema kuwa niliomba kuwa mbunge kwa lengo la kuwatumikia wananchi hivyo najitahidi huku na kule kuhakikisha natimiza azma yangu ya kuleta maendeleo kwa wananchi wa jimbo la Mufindi Kaskazini.

“Nimetoa jumla ya mifuko ya saruji 400 na bati 150 kwa ajili ya kuhamasisha ujenzi na ukarabati wa madarasa katika shule na zahati za kata hii ikiwa ni mwamzo tu nitaendelea kutoa saruji nyingine na bati hata vitu vingine ili kulifanya jimbo la Mufindi Kaskazini kupata maendeleo kwa kasi” alisema Mgimwa

Mgimwa alisema kuwa halmashauri ya Mufindi imeshaanda mpango kabambe ambao utakuwa msaada mkubwa kuchochoe maendeleo kwa kasi huku serikali ikiendelea kufanya jitihada za kuhakikisha wananchi wanapata maji ya kutosha na kuitumia vizuri ardhi ya halmashauri hiyo kwa kufanya maendeleo.

“Mimi lengo langu inapofika kipindi cha uchaguzi ninakuwa nimetatua kero zote za wananchi na kujihakikishia napewa ridha ya kuongoza kipindi kingine kwa maendeleo ya wananchi wa jimbo la mufindi kaskazini na kuongeza kuwa hatakusikia kuwa kuna kitu kinasababisha migogoro ya kugombea ardhi katika jimbo hili la Mufindi Kaskazini” alisema Mgimwa

Aidha Mgimwa alisema kuwa shule na zahanati zilizopata saruji na mabati ni shule za kijiji cha Mapanda,shule ya kijiji cha Uhafiwa,Ukama,Ihimbo na Chogo lengo ni kuchochoe kuleta maendeleo kwa wananchi.

Mgimwa amewapongeza wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo katika kata na ametoa ahadi ya kuendelea kushirikiana kwa kuchangia ujenzi wa shule zote za jimbo la Mufindi Kaskazini na kutatua kero nyingine za wananchi wa jimbo hilo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: