Aliyekuwa Mwenyikiti wa ACT-Wazalendo ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mgwhira akitangaza kuhamia CCM mapema leo katika mkutano huo wa tisa wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma.

 Aliyekuwa Mwenyikiti wa ACT-Wazalendo ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mgwhira akifungwa kiremba cha CCM mara baada ya kutangaza nia ya kuwa mwana- CCM 
 Mama Maria Nyerere akimpongeza aliyekuwa Mwenyikiti wa ACT-Wazalendo ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, mara baada ya kutangaza kuhamia CCM.
Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu akimpongeza aiyekuwa Mwenyikiti wa ACT-Wazalendo ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mgwhira mara baada ya kutangaza kuhamia CCM. PICHA NA IKULU.

Aliyekuwa Mwenyikiti wa ACT-Wazalendo ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mgwhira mapema leo hii ametangaza kujiunga na CCM alipokuwa katika Mkutano wa 9 wa Umoja wa Wanawake Tanzania UWT.

Mghwira amesema kuwa ameridhika na mwenendo mpya wa Chama hicho chini ya Mwenyekiti wake, Dkt John Pombe Magufuli.


”Nimeiona CCM inayobadilika, nimeona juhudi za kila mtu, ninaiona CCM inayoanza kukataa rushwa, nimeiona CCM inayoanza kulipeleka taifa mbele” amesema Anna Mghwira.


Mnamo Juni 3, 2017 Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania alimteua Anna Elisha Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Mghwira alikuwa mgombea pekee wa kike wakati wa kinyang’anyiro cha urais mwaka 2015, kwa tiketi ya chama cha ACT-Wazalendo na amekuwa mwenyekiti wa chama hicho tangu kilipoundwa mwaka 2014.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: