Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabulla akiteta na baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Ardhi Tabora.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabulla akiongea na wanafunzi na viongozi wa Chuo cha Ardhi Tabora.
Wanafunzi wa Chuo cha Ardhi Tabora wakimkisikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabulla alipokuwa akiwafafanulia jambo
.Wanafunzi wa Chuo cha Ardhi Tabora wakimkisikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabulla alipokuwa akiwafafanulia jambo.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabulla akikagua vifaa vya uchapaji na uandaaji wa ramani vya Chuo cha Ardhi Tabora vilivyogharimu kiasi cha milioni 200.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabulla akikagua vifaa vya uchapaji na uandaaji wa ramani vya Chuo cha Ardhi Tabora vilivyogharimu kiasi cha milioni 200.
Mkuu wa Chuo cha Ardhi Tabora Bwana Biseko Musiba akimuonesha mandhari ya Chuo cha Ardhi Tabora Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabulla.
---
Wanafunzi wa Chuo cha Ardhi Tabora wamekutana na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabulla na kumuomba atatue changamoto zinazowakabili.
Changamoto kubwa zilizoibuliwa na Wanafunzi hao ni suala la upatikanaji wa vifaa vya upimaji ardhi, uandaaji na uchoraji ramani, mafunzo ya vitendo, malazi na suala la uhakika wa ajira baada ya kumaliza masomo yao.
Wanafunzi hao walimueleza Mhe. Mabula adha wanayoipata katika kujifunza hasa wakati vinapohitajika vifaa vya upimaji na uandaaji ramani ambavyo kwa chuo hicho ni vichache na vina gharama kubwa kwao kuvimudu.
Katika kujibu hoja hizo Mhe. Mabulla alimtaka Mkuu wa Wilaya ya Tabora Bibi Queen Mwashinga na kumuagiza Mkuu wa Chuo cha Ardhi Tabora Bwana Biseko Musiba kuwatumia wanafunzi hao katika kuupanga mji wa Tabora na miji ya jirani na hasa katika katika kutatua migogoro ya ardhi.
Kuhusu vifaa vya upimaji ardhi, uandaaji na uchoraji ramani Mhe Mabulla alitembelea mitambo mipya ya uandaaji ramani ambayo kwa mujibu wa Mkuu wa Chuo imegharimu zaidi ya milioni 200 na ipo tayari kutumiwa na wanafunzi hao katika kujifunza.
Mkuu wa chuo hicho ameeleza kwamba vifaa hivyo vitatumiwa na wanafunzi hao katika mafunzo kwa vitendo na hata kutumika katika kuchora, kuandaa na kuchapisha ramani na machapisho mengine yenye ubora wa kutosha.
Kuhusu suala la ajira Naibu Waziri huyo aliwaambia wanafunzi hao kwa sasa serikali ya Mhe. Rais John Pombe Magufuli imejipanga kutatua migogoro ya ardhi na kuboresha taaluma ya ardhi, mipango miji, upimaji na ramani hivyo baada ya zoezi la uhakiki Serikali itaajiri maafisa hao kwa wingi. Hata hivyo wanafunzi hao wataendelea kutumiwa katika shughuli mbalimbali za upangaji mji wakati wakiwa chuoni kwa malipo maalumu.
Na katika hatua nyingine Mhe. Mabula ameliagiza Shirika la Nyuma la Taifa (NHC) mkoani tabora kushirikiana na ofisi ya Mkurugenzi wa Mji wa Tabora kujenga mabweni ya wanafunzi hao, nyumba za wafanyakazi na ofisi katika eneo linalomilikiwa na Chuo cha Tabora kwa kuzingatia mpango kabambe wa mji huo.
Kuhusu suala la kushughulikia migogoro iliyopo mkoani Tabora Mhe. Mabula ameuagiza Uongozi wa Manispaa ya Tabora kuhakikisha wanamaliza tatizo la uvamizi wa Viwanja vinavyomilikiwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) na vile vinavyomilikiwa na Taasisi nyingine na watu binafsi ili waweze kuviendeleza.
Kauli hiyo ameitoa wakati alipotembelea Ofisi za Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tabora akiwa katika ziara hiyo ya siku moja katika Chuo cha Ardhi Tabora.
Alisema kuwa ni vema Halmashauri zote zikahakikishe zinaondoa migogoro ya ardhi kwa kuhakikisha watu wenye maeneo yao ambayo yamevamiwa au kugawia watu wengine ambao sio wamiliki kihalali wanawaondoa na kuwarejeshea watu au Taasisi ambazo ndio zinazomiliki maeneo husika.
Toa Maoni Yako:
0 comments: