Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Gerson Lwenge akieleza maendeleo ya mradi wa maji Same - Mwanga. Mradi unaotoa maji bwawa la nyumba ya mungu.

Waziri Lwenge alieleza hatua nzuri ya maendeleo ya mradi na kuwa anayo imani kubwa kuwa mradi utamalizika Kwa muda uliopangwa - June, 2019. 

Pia aliweza kumtembelea mkandarasi anayejenga kipande cha Same akiongozana na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mngwira; ambapo pia mkandarasi alionekana ameanza vizuri. Aliwasisitiza wakandarasi wote kufanya kazi Kwa ubora na Kwa wakati.
Mradi huu mkubwa unategemea kisambaza maji miji ya Wilaya ya Same na Mwanga na baadaye vijiji 16 Same na Korogwe .

Mradi umegawanywa kwa wakandarasi 3. Ambapo eneo la Same Mkandarasi Badr amepewa kazi hiyo.

Kukamilika Kwa mradi huu ni sawa na kusema shida ya Maji Same baibai!!!.
Upatikanaji wa maji Same mjini utaongezeka kutoka 47% ya Sasa hadi kufikia 98%.

The green Same inakuja.

Pia Mhe. Waziri Lwenge akiongozana na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mngwira alipata nafasi ya kutembelea mradi wa maji Kizungo katika kata ya Vumari na aliahidi kuleta wataalamu toka Wizarani kujua sababu za kukwama Kwa mradi huo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: