Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa kairuki (tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe huo uliomtembelea ofisini kwake mapema leo. Picha na Ahmad Michuzi-China.
Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki akifafanua jambo alipokuwa akizungumza na Uongozi wa Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Mohamed Kiluwa (pichani kulia) pamoja na viongozi Waandamizi wa Serikali kutoka mkoa wa Pwani wakiongozwa na Katibu Tawala mkoa wa Pwani Zuberi Semataba, mapema leo kwenye Ofisi za Ubalozi huo,Ujumbe huo umewasili mjini Beijing,nchini China kushiriki Kongamano kubwa la uwekezaji wa Viwanda linalotarajiwa kufanyika mjini humo kesho Oktoba 25,2017.
Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki akifafanua jambo alipokuwa akizungumza na Uongozi wa Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies, Mohamed Said Kiluwa (pichani kulia) pamoja na Muwakilishi wa baadhi ya viongozi waandamizi wa mkoa wa Pwani,Katibu Tawala mkoa wa Pwani Zuberi Semataba waliofika mjini Beijing,nchini China kushiriki Kongamano kubwa la uwekezaji wa Viwanda linalotarajiwa kufanyika mjini humo kesho Oktoba 25,2017, Kongamano hilo limeandaliwa na Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies,litajumuisha wafanyashabiashara, wamiliki wa viwanda na makampuni wapatao zaidi ya 200 kutoka majimbo mbalimbali nchini China.
Katibu Tawala mkoa wa Pwani Zuberi Semataba akifafanua jambo mbele ya Balozi wa Tanzania nchini China,Mh. Mbelwa Kairuki mapema leo walipokwenda kumtembelea Ofisini kwake,pamoja na kupanga maandalizi ya Kongamano kubwa la uwekezaji wa Viwanda linalotarajia kufanyika mjini Beijing hapo kesho Oktoba 25,2017. Kongamano hilo limeandaliwa na Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies na kuwaalika viongozi Waandamizi wa Serikali ya Mkoa wa Pwani,wafanyabiashara wakubwa ambao ni wamiliki wa viwanda na makampuni mbalimbali.
Mkurugezi Mtendaji wa Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies, Naima Kiluwa akiandika kilichokuwa kikijiri kwenye mazungumzo hayo mafupi na Balozi Mh.Mbelwa Kairuki mara baada ya kuukaribisha ujumbe huo Ubalozini kwake na kuzungumza mambo mbalimbali yaliyohusu masuala ya uwekezaji kwa Tanzania,na baadae kupata chakula cha pamoja.
Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki akimkabidhi zawadi mmoja wa watakaoshiriki Kongamano la Viwanda linalotarajia kufanyika kesho mjini Beijing,likatalojumuisha Wamiliki wa Viwanda,Wafanyabiashara kutoka sehemu mbalimbali wapatao zaidi ya 200,anaeshuhudia kushoto ni Katibu Tawala mkoa wa Pwani, Zuberi Semataba
Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa kairuki akimkabidhi zawadi Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies, Mohamed Said Kiluwa.
Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki akimkabidhi zawadi Mkurugezi Mtendaji wa Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies, Naima Kiluwa.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies,Mohamed Said Kiluwa akiwatambulisha baadhi ya washirika wake mbele ya Balozi Kairuki (hayupo pichani), mapema leo mjini Beijing nchini China,wakiwa tayari kwa maandalizi ya Kongamano la Uwekezaji wa Viwanda linalotarajia kufanyika hapo kesho Octoba 25, 2017 mjini humo.
Rais wa wanafunzi wasomao nchini China, Hussein Mtoro akiukaribisha Ujumbe kutoka Serikali ya Mkoa wa Pwani ikiongozwa na Katibu Tawala mkoa wa Pwani, Zuberi Semataba pamoja na uongozi wa Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies ukiongozwa na Mohamed Said Kiluwa (njano), walipofika Ofisini kwa Balozi wa Tanzania nchini China, Mhe. Mbelwa Kairuki, mapema leo mchana.
Kongamano hilo kubwa lenye uhamasishaji mkubwa wa uwekezaji wa Viwanda nchini Tanzania,limeandaliwa na Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies na litawashirikisha wafanyabiashara, wamiliki wa viwanda na makampuni wapatao zaidi ya 200 kutoka majimbo mbalimbali nchini China.
Balozi Kairuki amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies Mohamed Kiluwa kwa kuonesha juhudi kubwa za kuwahamasisha na kutafuta washirika mbalimbali katika suala zima la uwekezaji wa viwanda nchini Tanzania.
Balozi Kairuki amesema kuwa,Kampuni ya Kiluwa kwa kufanya hivyo wanaibeba dhana ya Tanzania ya Viwanda kwa utekelezaji kwa vitendo,na pia kuunga mkono dhamira ya Rais Dkt John Pombe.
Magufuli ya kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi ya Viwanda,na kuongeza kuwa yuko tayari kutoa kutoa ushirikiano wa kutoka katika suala zima la kuwahamasisha wawekezaji kutoka nchini China na kwenda kuwekeza nchini tanzania katika suala zima la Viwanda.
Toa Maoni Yako:
0 comments: