Meneja Mauzo Kanda ya Dar es Salaam Airtel Tanzania Brighton Majwala (kulia) akimkabidhi vifaa vya mchezo Katibu Mkuu wa Chama cha Soka wilaya ya Kinondoni (KIFA) Funia A. Funia (kushoto) kwa ajili ya mashindano ya Chipukizi Cup yanayotarajiwa kuanza Octoba 8 kwenye viwanja vine vya wilaya hiyo. Wa pili kushoto ni Katibu wa mashindano ya vijana wa wilaya hiyo Abdallah Singano na Meneja Miradi Airtel Tanzania Jane Matinde.
Katibu wa soka la vijana wa wilaya ya Kinondoni Adballah Singano (kushoto) akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam baada ya kukabidhiwa vifaa vya michezo na kampuni ya simu za mkononi Airtel Tanzania kwa ajili ya mashindano ya Chipukuzi Cup yanayotarajiwa kuanza Octoba 8. Kulia ni Meneja Miradi Airtel Tanzania Jane Matinde na katikati ni Katibu wa Chama cha Soka wilaya ya Kinondoni (KIFA).
---
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetoa msaada wa vifaa vitakavyotumika kama zawadi katika mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 yajulikanayo kama Chipukizi Cup yanayotegema kutimua vumbi tarehe 8 october 2017 katika wilaya ya kinondoni
Mashindana hayo yanayoshirikisha timu 64 kutoka katika wilaya ya Kinondoni yatatoa fursa kwa vijana kuchuana vikali , kujifua na kujiweka sawa katika kuchezea vilabu mbalimbali na hatimae kukuza kiwango cha mpira nchini
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo Meneja Masoko kanda ya Dar es saalam , Brighton Majwala alisema “ leo hii tunaungana na chama cha mpira wa soka wilaya ya Kinondoni katika kudhamini mashindano haya kwa lengo la kuwapatia vijana jukwaa la kuonyesha vipaji vyao na kujiweka sawa katika mchezo wa Soka. Kwa miaka 7 mfululizo tumekuwa tukiendesha mashindano ya mpira kwa vijana kupitia program yetu ya Airtel Rising Stars na leo tumeona ni vyema kuwafikia vijana mitaani kwa kudhamini mashindano ya mpaira wa miguu katika ngazi ya wilaya ili kuwezesha vijana wengi kuonyesha vipaji vyao na kutumiza ndoto zao”.
“Tunaushukuru uongozi wa mpira wa wilaya ya kinondoni kwa kutualika kushiriki nao ni matumaini yetu kupitia mashindano haya tutaweza kuwaunganisha vijana pamoja, kuchochea kukua kwa mpira wa soka nchini lakini pia kuamashisha mashindano ya mitaani yaweze kufanyika na kuwa na mvuto Zaidi huku vijana wengi Zaidi wakipata nafasi ya kushiriki
Tunatoa wito kwa vijana na timu zilizojiandikisha kutumia fursa hii vyema kwani mpira wa miguu ni ajira na njia ya kupata kipato. Airtel tutaendelea kushirikiana na viongozi wa soka katika wilaya mbalimbali nchini katika kuhakikisha tunatoa nafasi kwa vijana kushiriki mashindano kama haya na kuwajenga Zaidi na kuwafanya wawe wanasoka bora ndani na nje ya nchi ”
Kwa upande wake Mwenyekiti wa soka la vijana wilaya ya Kinondoni, Abdallah Singano alisema “ Tunawashukuru sana Airtel kwa kukubali kudhamini mashindano haya kwa kutoa zawadi za washindi. Ushiriki wa Airtel umeongeza mvuto wa mashindano haya na mwitikio umekuwa mkubwa sana. Hadi sasa tunazo timu 64 ambazo zimekwisha jiandikisha siku ya Jumamosi na Jumapili ili kushiriki mashindano haya, usajiri huu ulifanyika katika viwanja vya KIFA Mburahati, Msasani CCM magunia, Mwananyamala ETIHAD pamoja na uwanja wa Tegeta. Timu zote ziko tayari na sisi kama wasimamizi wakuu wa mashindano haya tumejipanga kusimamia vyema mashindano haya ili yaweze kuendelea kuleta tija katika soka letu”
Napenda kutoa wito kwa wapenzi wa mpira mashabiki kujitokeza kwa wingi kufatilia michuano hii pindi itakapoanza kutimua vumbi hapo tarehe 8 octoba katika viwanja mbalimbali wilayani Kinondoni, ratiba kamili ya mashindano hayo itatolewa pindi itakapokamilika”
Katika michuano hiyo Airtel imetoa zawadi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Jezi, kombe, Soksi , shin guard, Tshirts, medali, pamoja na zawadi mbalimblai kwa wachezaji bora wa michuano hiyo. Jumla ya Zaidi hizo zina dhamani ya shilingi million 5.
Toa Maoni Yako:
0 comments: