Kamishna Jenerali wa Idara ya Uhamiaji Dk. Anna P. Makakala wa kwanza kutoka kushoto akikagua vichochoro vinavyotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini katika kijiji cha Mugulika Kata ya Bwerenyange wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera. Kamishna Jenerali yuko mkoa wa Kagera kujionea shughuli zinazotekelezwa na Idara yake mkoani humo.
Kamishna Jenerali wa Idara ya Uhamiaji Dk. Anna P. Makakala wa kwanza kutoka kushoto akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Karagwe mkoa wa Kagera Godfrey Mheluka watatu kutoka kulia katika kijiji cha Muguluka Kata ya Bwerenyange wilaya ya Karagwe Mkoa wa Kagera. Kamishna Jenerali huyo amefanya ziara katika Vipenyo vinavyotumiwa na wahamiaji haramu kutoka nchini nyingine kuingia Tanzania.
Kamishna Jenerali wa Idara ya Uhamiaji Dk. Anna P. Makakala wa nne kutoka kulia akiwa katika Mkutano wa Hadhara na baadhi ya Wananchi (hawapo pichani) wa Kijiji cha Muguluka Kata ya Bwerenyange wilaya ya Karagwe Mkoa wa Kagera.Kamishna Jenerali huyo amefanya ziara katika Vipenyo vinavyotumiwa na wahamiaji haramu kutoka nchini nyingine kuingia Tanzania.
Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Muguluka Kata ya Bwerenyange wilaya ya Karagwe Mkoa wa Kagera wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa Idara ya Uhamiaji Dk. Anna P. Makakala katika Mkutano wa Hadhara baina ya wanakijiji hao na Ujumbe huo wa Idara ya Uhamiaji kutoka Makao Makuu ambapo katika Mkutano huo Dk. Makakala alitoa wito kwa wanakijiji hao kutowahifadhi wahamiaji haramu kwenye makazi yao sambamba na kuwataka kutoa taarifa kwenye vyombo vya dola pale wanapogundua kuna mgeni asiyeeleweka na wanamtilia mashaka kwenye makazi yao.(Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
Toa Maoni Yako:
0 comments: