Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Chama Cha Ushiriki Wilayani Ikungi Cha AMINIKA kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi.Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu pamoja na viongozi wengine wakifatilia taarifa ya Chama Cha Ushiriki Wilayani Ikungi Cha AMINIKA wakati wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa Bodi ya Wakurugenzi.
Baadhi ya Wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Chama Cha Ushiriki Wilayani Ikungi Cha AMINIKA wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu.
Katibu wa Bodi ya Wakurugenzi ya wachimbaji wadogo wadogo ya AMINIKA Ndg Hamisi Nkingi akisoma taarifa ya wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa Bodi hiyo kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi.
Na Mathias Canal, Singida
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu amekubali ombi la viongozi wa Chama Cha Ushiriki Wilayani Ikungi Cha AMINIKA la kuwa mlezi wao Sambamba na kuchangia Shilingi Milioni Moja kwa ajili ya kusaidia Kupunguza ukali wa changamoto zinazowakabili.
Chama hicho Cha USHIRIKA wa wachimbaji wadogo (AMINIKA GOLD MINE CO-OPERATIVE SOCIETY LTD) chenye jumla ya wanachama 193 Ni muungano wa vikundi vitano vya Uchimbaji mdogo wa Madini ya dhahabu vinavyotokana na vikundi vya Elimika-Sambaru, Amka-Sambaru, Amani-Sambaru, Aminifu-Mang'onyi na Muungano-Mlumbi.
Akizungumza na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya AMINIKA Mhe Mtaturu alimuagiza Afisa Ushirika wa Wilaya ya Ikungi Ndg Gurisha E. Msemo kutoa taarifa ya kila mwezi kuhusu mwenendo wa Chama hicho.
Alisema kuwa Uongozi wa Wilaya unatambua umuhimu wa Chama hicho kutokana na umahiri wake na muelekeo wa kuwakomboa wachimbaji wadodo katika Wilaya ya Ikungi.
Alisema ili Chama hicho kuwa na Ushirika mzuri na mafanikio makubwa Ni vyema viongozi watakaochaguliwa kutanguliza maslahi ya wananchi mbele kwa kusoma taarifa kwa uwazi na ukweli.
Mhe Mtaturu alisema mafanikio ya Chama Cha Ushirika Cha AMINIKA Ni pamoja na kuchagua viongozi Bora watakaokuwa na mikakati makini kea ajili ya kukikomboa Chama na kuwa na mbinu zenye manufaa kwa ustawi wa Chama.
Uchaguzi wa Viongozi wa Bodi ya Chama hicho Cha USHIRIKA Cha wachimbaji wadogo (AMINIKA GOLD MINE CO-OPERATIVE SOCIETY LTD) kinafanya uchaguzi wa awamu ya Pili kwa kipindi Cha miaka mitatu 2017/2020 mara Baada ya Uongozi uliopo madaraka kumaliza muda wake kwa kipindi Cha awamu ya kwanza Mwaka 2014/2017.
Toa Maoni Yako:
0 comments: