Kaimu Mkurugenzi wa PSPTB Bw. Godfred Mbanyi akizungumza na wanafunzi waliofikia Level 5 wanaotarajiwa kufanya mitihani ya Bodi ya Wataalam wa Ununuzi Ugavi katika Warsha ya Mafunzo ya siku ya Utafiti iliyondaliwa na Bodi hiyo ambapo kila mwanafunzi atapangiwa msimamizi wa utafiti wake na baadaye utafiti wao utapimwa kitaalamu ambapo utawawezesha kuwa wataalamu wa masuala ya Ununuzi wa Umma baada ya Kupata cheti cha kitaaluma cha (CPSP)
Bw. Godfred Mbanyi amewataka wanafunzi hao kuwa wasikivu wakati wa mafunzo hayo, lakini pia amewaasa kuwa na maadili ya kazi zao, Amesema pamoja na kusoma na kuwa na vyeti lakini kama hawatakuwa na maadili hawatakuwa na umuhimu wowote kwa bodi na kwa nchi kwa ujumla.
Mbanyi ameongeza kwamba "Wakimalizia mitihani yao na kufaulu tutawaapisha kiapo cha maadili na kiapo hicho tutakitumia mahakamani kama ushahidi endapo hawatafuata maadili katika kazi zao na kuifedhehesha Bodi ya PSPTB) kwa kufanya mambo bila kufuata utaratibu wa sheria zinazozimamia Ununuzi wa Umma".
Amemaliza na kusema kwamba Wataalamu wa masuala ya Ununuzi wa Umma wanashikilia fedha nyingi za serikali lakini watambue kwamba fedha hizo ni za watanzania na wanatakiwa kuzitumia vizuri kwa kufuata utaratibu uliowekwa ili ziwe na manufaa kwa watanzania wote katika kuondokana na changamoto mbalimbali zinazokwamisha maendeleo ya nchi na watanzania kwa ujumla, warsha hiyo inafanyika kwenye ukumbi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima jijini Dar es salaam
Kaimu Mkurugenzi wa PSPTB Bw. Godfred Mbanyi akifafanua jambo wakati alipokuwa akizungumza na wanafunzi wanaotarajiwa kufanya mitihani ya Ununuzi wa Umma iliyofanyika kwenye ukumbi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima jijini Dar es salaam, Kulia ni Amani Ngonyani Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo PSPTB na kushoto ni Mkufunzi wa Mafunzo hayo Dk Ikandilo Kushoka.
Amani Ngonyani Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo PSPTB akizungumza katika warsha hiyo katikati ni Bw. Godfred Mbanyi Kaimu Mkurugenzi wa PSPTB na kushoto ni Mkufunzi wa Mafunzo hayo Dk Ikandilo Kushoka.
Bw. Godfred Mbanyi Kaimu Mkurugenzi wa PSPTB akifafanua jambo katika warsha hiyo kushoto ni Mkufunzi wa Mafunzo hayo Dk Ikandilo Kushoka na kulia ni Amani Ngonyani Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo PSPTB.
Baadhi ya washiriki wa Warsha hiyo wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa PSPTB Bw. Godferd Mbanyi hayupo pichani wakati alipokuwa akizungumza nao.
Wanafunzi hao wakisikiliza kwa makini.
Toa Maoni Yako:
0 comments: