Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, akipokea
vifaa vya kuzuia vumbi kwa askari wa usalama barabarani kutoka kwa
msamaria mwema, Tahir Othman (kulia) ,aliyejitolea vifaa hivyo ili
kusaidia askari kuepukana na vumbi kuingia kwenye njia ya hewa wawapo
katika shughuli zao.Anayeshuhudia katikati ni Naibu Waziri Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la
Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni .Makabidhiano hayo
yamefanyika ofisini kwa Naibu Waziri,jijini Dar es Salaam. Picha na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, akionyesha
kwa waandishi wa habari jinsi ya kuvaa kifaa cha kuzuia vumbi kwa
askari wa usalama barabarani alivyopokea kutoka kwa msamaria
mwema,Tahir Othman(hayupo pichani) ,aliyejitolea vifaa hivyo ili
kusaidia askari kuepukana na vumbi kuingia kwenye njia ya hewa wawapo
katika shughuli zao.Kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama
Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni. Makabidhiano hayo yamefanyika
ofisini kwa Naibu Waziri, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi.
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI


Toa Maoni Yako:
0 comments: