Watoto wa wafanyakazi wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel, wakifurahia ndani ya bwawa la kuogelea katika shamrashamra za siku ya wanafamilia wa Airtel jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wafanyakazi na familia zao wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel wakichukua chakula kwa pamoja kuonyesha upendo na mshikamano wao ambao ni sehemu ya mafanikio ya kampuni hiyo wakati wa hafla ya Siku ya Wanafamilia wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana.
Mwanafamilia wa Airtel akiwapa chakula watoto ikiwa ni ishara ya upendo ulio ndani ya wafanyakazi wa kampuni hiyo wakati wa hafla ya Siku ya Wanafamilia wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana.

Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel Tanzania yasherehekea siku ya wanafamilia mwishoni mwa wiki hii Kunduchi Wet n Wild .

Ni muda muafaka kwa familia mbali mbali kuwezakujuana na kujumuika kwa pamoja na kuweza kubadilishana mawazo na hata kufurahia mafanikia ya matunda waliyoyapata kwa mwa huu.

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Airtel Tanzania, Patrick Foya alisema ni desturi yao kuwa na siku maalumu kila mwaka ya kuwakutanisha wafanyakazi wao na familia zao ili pamoja na kushiriki michezo na mambo mengine ya kuburudisha nyoyo zao zao lakini pia huitumia siku hiyo kuzidi kuimarisha mshikamano miongoni mwao. "Umoja na mshikamano ni nyenzo muhimu mahali pa kazi, lakini pia ukiwa na mfanyakazi anayetoka katika familia iliyokosa utulivu, lakini pia mfanyakazi legelege hawezi kufanya kazi zake kwa ufanisi," akaongeza Bwana Foya.

Zaidi ya wafanyakazi na wanafamilia 600 walishiriki katika bonanza hilo na kushiriki michezo mbalimbali kama vile kucheza muziki, kuvutaka kamba, soka la baharini, wavu na kuogelea. Baadhi ya watoto wa wafanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania wakishindana.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: