MAAMUZI YA BARAZA KUU LA UONGOZI TAIFA LA CUF lililokutana leo Zanzibar:

Na Julius Mtatiro. 

1. Limemfukuza uanachama, Prof. Ibrahim Haruna Lipumba baada ya kujiridhisha kuwa amekiuka katiba ya chama kwa kuvamia Ofisi Kuu ya chama, kuongoza makundi ya wahuni yaliyopiga walinzi wa chama, kuvunja ofisi za chama na kufanya uharibifu wa mali za chama siku ya tarehe 24 Septemba 2016. (Baraza limejiridhisha kuwa Kikao cha Kamati ya Utendaji kiliitishwa kwa kufuata masharti ya Katiba na hakikuvunja masharti yoyote ya kuitisha Baraza Kuu na limejiridhisha kuwa Prof. Lipumba alifikishiwa barua yenye tuhuma zake lakini kwa makusudi amekiuka kuitikia wito wa baraza na hivyo kujipotezea haki ya kusikilizwa).

2. Limeukataa ushauri na mwongozo wa Msajili wa Vyama vya siasa alioutoa kwa chama kwa sababu umekiuka matakwa ya Sheria ya Vyama Vya Siasa ya Tanzania, hauna mantiki na mashiko ya kisheria na unakiuka matakwa ya katiba ya CUF.

3. Limesisitiza kuwa Kamati ya Uongozi liliyoiunda ndiyo inayotambulika kikatiba hadi hapo atakapochaguliwa Mwenyekiti mpya wa CUF.

MY TAKE;
Chama cha siasa huendeshwa kwa vikao halali siyo maamuzi na matakwa ya mtu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: