RSM, Mtandao wa Kimataifa katika ukaguzi wa mahesabu na tathmini za kodi, umesherehekea madhimisho tano ya kila mwaka ya Siku Maalumu Duniani ya RSM—kwa kuchangia madawati kwa shule mbalimbali za Dar es Salaam.
Mchango wa RSM, Mtendaji Mkuu wa RSM Afrika Mashariki, Bi. Lina Rantasi alisema kuwa timu ya RSM imedhamiria kusaidia jitihada za Serikali za kuokoa maisha na kuendeleza elimu.
Bi. Ratansi aliendelea kusema,”Kumekuwa na wito mwingi wa kuchangia madawati, Na sisi hatutaki kubaki nyuma, ndo maana tumetoa madawati 50 (3, 750, 000) ili kusaidia watoto wasika chini tena.”
Amesema madawati utasaidia kuongeza uwezo na akili za watoto katika masomo, hivyo kuongeza ufaulu, kwa sababu “motto akikaa chini hata ufahamu wake unakuwa mdogo.
Akipokea madawati hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Madawati-Mkoa wa Dar es Salaam, Hamid Abdul Rahaman, amesema mchango wa RSM utasaidi kukuza sekta ya elimu, na kuwapongeza Mtandao wa RSM kwa kuunga mkono kampeni ya kitaifa ya kuziwezesha shule kuwa na madawati ya kutosha.
Toa Maoni Yako:
0 comments: