Mkuu wa wilaya ya Muheza Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza na bodaboda wa wilaya hiyo ambapo alikutana nao na kuzungumza nao kwenye uwanja wa Jitegemee wilayani humo ambapo alipiga marufuku kuendeshwa usiku zaidi ya saa sita.
Katibu Tawala wa wilaya ya Muheza (Das) akizungumza katika mkutano huo kabla ya kumkaribisha Mkuu wa wilaya hiyo, Hajat, Mhandisi Mwanasha Tumbo aliyekaa kushoto na anayefuata ni Mwenyekiti wa Waendesha Boda Boda wilayani Muheza.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza ambaye pia ni Afisa Biashara wa wilaya hiyo, Ally Mokiwa akielezea namna walivyojipanga kuhakikisha waendesha bodaboda hao
wanakata leseni za kuendesha shughuli zao katikati ni Mkuu wa wilaya ya Muheza, Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo.
wa pili kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Muheza, Hajat, Mhandisi Mwanasha Tumbo akimsikiliza kwa umakini Mkuu wa Usalama Barabarani wilayani Muheza (DTO) Herbert Kazonde wakati wa mkutano huo na waendesha bodaboda uliofanyika kwenye uwanja wa Jitegemee wilayani humo kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Muheza.
Katibu wa Chama cha Waendesha Boda Boda wilayani Muheza, Francis Gerald akizungumza katika mkutano huo kuhusu changamoto ambazo zinawakabili.
Madereva wakiwa kwenye kikao chao na Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga, Mhandisi, Hajat Mwanasha Tumbo. Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.
Toa Maoni Yako:
0 comments: