Multichoice yakabidhi vifaa maalum vya michezo kwa watu wasioona ambavyo vitawawezesha kuhudhuria maadhimisho ya siku ya kimataifa ya fimbo nyeupe tarehe 06/10/2016 itakayofanyika mkoani Mbeya. Lengo kuu la maadhimisho hayo ni kuhamasisha jamii na watumiaji wa barabara, kuiheshimu fimbo nyeupe, na kumsaidia asiyeona anapotembea na anapohotaka kuvuka barabara.
Vifaa vilivyotolewa ni: Mipira (4) ya goalball, Domino set nne, Karata nne, fedha za nauli na kujikimu kwa timu hiyo ya wasioona. Mchango huo wa Multichoice unathamani ya jumla ya shilingi 3,120,000/=. Akitoa msaada huo mkurugenzi mkuu wa Multichoice Tanzania Maharage Chande alisema “Multichoice inafuraha kubwa kushirikiana na nduguzetu wasioona wa Dar es salaam katika kuwaandaa kushiriki maadhimisho yatakayofanyika Mbeya, kama kampuni ya kitanzania tutaendelea kuwa mstari wa mbele kushirikiana na jamii yetu kila fursa inapojitokeza”.
Kampuni ya MultiChoice Tanzania inaomgoza kwa kutoa burudani za michezo na filamu kwa kupitia DSTV. Makao makuu yake ni Dar es salaam na Inamatawi Mwanza, Arusha, na Mbeya.
Toa Maoni Yako:
0 comments: